Monday 18 July 2016

OSHARA YAONGOZA MATOKEO KIDATO CHA SITA WILAYA YA SIHA 2016


shule ya Sekondari ya Serikali Oshara yashika nafasi ya Kwanza katika matokeo ya kidato cha sita  Wilaya ya Siha na kuzishinda shule binafsi na za taasisi za Dini Wilayani Siha.
baadhi ya Shule zenye majina  makubwa zilizopitwa na shule hii ni pamoja na shule ya Masista Visitation Girls Sekondari na shule ya Sekondari Faraja Siha.

matokeo ya shule za Sekondari Wilaya ya Siha kwa mtihani wa kidato cha Sita mwaka 2016 yaliyotangazwa hivi karibuni:

1. SHULE YA SEKONDARI OSHARA: DIV I=8,DIV II=36,DIV III=05,nafasi ya kwanza Kiwilaya,6 Kimkoa (6/50) na 44 Kitaifa(44/423)

2.MAGADINI SEKONDARI: DIV I=09,DIV II=32,DIV III=10, nafasi ya Pili Kiwilaya ,10 Kimkoa(10/50),59 Kitaifa(59/423)

3.VISITATION GIRLS SEKONDARI: DIV I=4,DIV II=35,DIV III=15,Nafasi ya 14 kimkoa(14/50),113 Kitaifa(113/423)

4.SANYA JUU SEKONDARI: DIV I=07, DIV II=29,DIV III=36,DIV 4=12,DIV 0=02 nafasi 41 Kimkoa(41/50),331 Kitaifa(331/423)

5. FARAJA SIHA:DIV I=1,DIV II=09,DIV III=32,DIV 4=6 nafasi 47 Kimkoa(47/50),369 Kitaifa (369/423)

shule za Siha zafanya kweli matokeo kidato cha Sita mwaka 2016


Shule za sekondari za Serikali Wilayani Siha zimepata matokeo mazuri ya  kidato cha sita (form Six kwa mwaka 2016) na kushangaza shule nyingi kongwe mkoani Kilimanjaro.
shule zilizofanya vizuri katika matokeo hayo ni;-

OSHARA SEKONDARI: Matokeo yake Div 1=8,Div II=36,Div III=05 hakuna four wala Zero. shule hii imeshika nafasi ya kwanza Wilaya ya Siha kati ya shule tano zilizopo(1/5) ,nafasi ya 6 mkoa wa Kilimanjaro kati ya shule 50(6/50) na nafasi ya 44 kitaifa kati ya shule 423

Aidha, shule nyingine iliyofanya mtihani wa Kidato cha Sita na kushangaza wengi ni MAGADINI SEKONDARI.Matokeo ya shule hii ni kama ifuatavyo:Div I=09,Div II=32,DivIII=10.hakuna daraja la 4 wala sifuri. Shule hii imeshika nafasi ya 2 Kiwilaya kati ya Shule 5,nafasi ya 10 Kimkoa kati ya shule 50 na nafasi ya 59 kati ya shule 423

Saturday 16 July 2016

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA SIHA ARIPOTI OFISINI RASMI

 Mkurugenzi mpya wa Wilaya ya Siha Ndg Valerian Juwal aripoti ofisini rasmi


JAJI MKUU WA TANZANIA AZINDUA MAHAKAMA YA WILAYA YA SIHA







RC KILIMANJARO AWATAKA MADIWANI SIHA KUSIMAMIA MAPATO

 mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Said Meck Sadiki akizungumza na Baraza la Madiwani Wilayani siha katika mkutano maalum wa Baraza hilo

KAMBI YA TAIFA YA WANARIADHA YATEMBELEWA WILAYANI SIHA NA NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO


naibu Waziri wa habari ,utamaduni,sanaa na michezo Mh.Anastazia Wambura akiwa na wanariadha wa Tanzania waliopiga kambi West Kilimanjaro. wanariadha hao wanajiandaa na mashindano ya Olympic yatakayofanyika Brazil mwaka huu

MH NAPE AZINDUA SHEREHE ZA KIMILA WILAYANI SIHA-KILIMANJARO


Mh Nape Nnauye waziri wa habari,utamaduni ,sanaa na michezo akihuhubia wananchi na wanamila wa kabila la kimasai alipokuwa Wilayani siha

NAPE APOKELEWA KWA KISHINDO NA VIONGOZI WA KIMILA SIHA

 WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO MH.NAPE M.NNAUYE AKIKARIBISHWA NA VIONGOZI WA WILAYA YA SIHA NA VIONGOZI WA KIMILA WA KIMAASAI KUFUNGUA SHEREHE ZA KUKABIDHI RIKA KWA KABILA HILO MAARUFU AFRIKA NA DUNIANI KWA UJUMLA. SHEREHE ZIMEFANYIKA KIJIJI CHA ORMELILI WILAYA YA SIHA MKOA WA KILIMANJARO


DC SIHA AKABIDHIWA OFISI RASMI

 Mkuu mpya wa Wilaya ya Siha mh. Onesmo Buswelu (kushoto) akipokea nyaraka za kukabidhiwa ofisi hiyo na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Dr. Charles Mlingwa ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara
 Mh. Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha akisaini hati ya makabidhiano ya ofisi

DC SIHA ATAMBULISHWA RASMI SIHA

 MKUU MPYA WA WILAYA YA SIHA MH .ONESMO BUSWELU  AKIJITAMBULISHA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA FEDHA,UONGOZI NA MIPANGO HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA.HII NI BAADA TU YA KUAPISHWA KUSHIKA WADHIFA HUO

MKUU MPYA WA WILAYA YA SIHA AAPISHWA RASMI

 MKUU WA WILAYA YA SIHA MH.ONESMO BUSWELU AKILA KIAPO KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

Friday 15 July 2016

HALMASHAURI YA SIHA YAENDELEA KUPATA HATI SAFI





Siha yapongezwa kwa kupata Hati Safi
Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro imepongezwa kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya mkaguzi  na mthibiti Mkuu  wa hesabu za Serikali

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki wakati alipohudhuria kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Siha kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo katikati ya Juma. 

Mkutano huo maalum uliitishwa kwa agenda moja ya kupitia ripoti ya Mkaguzi na mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha 2014/2015.

Katika Mkutano huo maalum wa Baraza la Madiwani, mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro aliwapongeza Baraza la Madiwani la kipindi kilichopita kwa usimamizi mzuri wa shughuli za Serikali hasa rasilimali fedha

Alieleza kuwa hati safi inapatikana baada ya kila mtu kutimiza wajibu wake, na hivyo aliwataka Madiwani wa Halmashauri ya Siha  kama wasimamizi wakuu wa shughuli za maendeleo wahakikishe wanasimamia kwa ukaribu fedha zote zinazotumwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ndugu zangu kama halmashauri itashindwa kukusanya mapato ya kutosha kitakachoendelea ni kushindwa  kujiendesha na  ninyi kama Madiwani mtakuwa mmeshindwa kutimiza  wajibu wenu na mnaweza kusababisha Halmashauri yenu kufutwa kama lilivyo agizo la Serikali ”alisema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
“Mimi pamoja na Mkuu wenu wa Wilaya ya Siha kama wasimamizi wa Halmashauri tutaendelea kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanatekelezwa katika viwango vinavyostahili hasa usimamizi wa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara,miundombinu ya maji ,Elimu na shughuli nyingine zote” alibainisha Meck Sadiki

Awali akiwasilisha ripoti hiyo ya Mkaguzi na Mthibiti mkuu wa Hesabu  za Serikali, Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo  Peter Temba aliliambia Baraza  kuwa, Halmashauri ya Siha ni miongoni mwa Halmashauri 49 hapa Nchini na miongoni mwa Halmashauri mbili pekee katika Mkoa wa Kilimanjaro  zilizopata hati safi kwa mwaka 2014/2015

Alieleza kuwa hii,imetokana na ushirikiano mzuri uliokuwepo kati ya wasimamizi wa Halmashauri yaani baraza la Madiwani na Wataalam wa Halmashauri pamoja  na Wananchi na Wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya wilaya hiyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha imekuwa ikifanya vizuri katika usimamizi wa fedha za maendeleo na kufanya halmashauri hiyo kupata hati safi kwa zaidi ya miaka saba mfululizo tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2007

MKURUGENZI MPYA SIHA ARIPOTI OFISINI RASMI

baada ya uteuzi wa Wakurugenzi wapya na kula kiapo Ikulu Tarehe 12.7.2016 uliofanywa na  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ndugu VALERIAN M. JUWAL ameripoti ofisini tarehe 15.7.2016 na kuanza kazi Rasmi