Thursday 29 December 2016


Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe.Onesmo Buswelu akisikiliza kero mbalimbali za wananchi katika kijiji cha Namwai Kata ya Ngarenairobi  hivi karibuni

Baadhi ya wananchi wakitoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya ya Siha wakati alipofanya ziara mfupi katika kijiji cha Namwai.



Wednesday 28 December 2016

Barabara ya Lami Sanya Juu kamwanga kuanza kujengwa hivi karibuni

 Baadhi ya mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Barabara ya Lami sanya Juu kamwanga.awamo ya kwanza zitajengwa km 32.5 sanya Juu hadi Elerai (picha ya mpiga picha wetu)

 Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO Mhe. Saidi Meck Sadick kulia hapo Juu akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha wakati wakitembelea kambi ya ujenzi wa Barabara ya Sanya Juu Kamwanga .ukaguzi ulifanyika tarehe 28.12.2016

Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO Saidi Meck  Sadick akikaribishwa  na wakandarasi wa Barabara hiyo raia wa nchini China


Baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Siha Magharibi wakimsikiliza mhe. Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO Jana alipokuwa kijiji cha Ngarenairobi kwa lengo la kuwatambulisha wakandarasi wataojenga Barabara ya Sanya Juu Kamwanga kwa kiwango cha Lami

Monday 14 November 2016

Habari katika picha


Moja ya jengo la Hospital mpya ya Wilaya ya Siha eneo la Kata ya Sanya Juu

Misitu wa kupandwa Shamba la miti West KILIMANJARO karibu la lango la kupanda kilele cha mlima KILIMANJARO Londorosi

Friday 4 November 2016

Thursday 3 November 2016

UHIFADHI ya mlima KILIMANJARO kupitia lango la Londorosi Geti Wilayani SIHA

Muonekano wa mlima kituo cha Shira Wilayani SIHA kupitia lango la Londrosi


Kilele cha mlima KILIMANJARO kikiwa kimezungukwa NA barafu Kali kama kinavyoonekana katika kituo cha Shira kupitia lango la Londrosi Wilayani SIHA_KILIMANJARO

KILIMO cha kuiga katika MAENEO yetu


Namna ya kutunza mboga za majani aina ya sukuma katika mifuko MAENEO ya nyumbani

UJUNZAJI wa MAJI katika KILIMO cha migomba kwa kufunika ardhi kwa kutumia majani

KILIMO bora cha nyanya kinashauriwa kuwa hivi kama inavyoonekana katika picha(picha ya maktaba yetu)

Shamba la migomba linatakiwa kuwa safi NA idadi ya migomba katika shina moja  inatakiwa kuwa miwili au mitatu mwisho(picha nanenane 2016)
Uvunaji wa MAJI ya mvua unasaidia kupunguza matumizi ya MAJI NA kuondoa upoteaji wa MAJI usio wa lazima HASA MAENEO ya makazi

Wednesday 2 November 2016

Uboreshaji wa makazi ya walimu Wilayani Siha


Moja ya nyumba za walimu zilizozinduliwa NA mwenge wa Uhuru Wilayani Siha mwaka 2016(picha ya maktaba yetu)

Wajumbe wa Kamati ya ushauri ya Wilaya ya SIHA yakutana kwa kikao cha kawaida.



Wajumbe wa kamati ya ushauri ya Wilaya ya SIHA wakiwa katika kikao cha kawaida cha kamati hiyo. Kikao kinaendelea katika ukumbi wa mikutano wa HALMASHAURI ya Wilaya ya SIHA

Wajumbe wa DCC -wilayani SIHA wakiendelea NA kikao cha kawaida katika ukumbi wa mikutano wa HALMASHAURI ya SIHA muda huu

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya SIHA chafanyika leo tarehe 2.11.2016


Mkuu wa Wilaya ya SIHA Mhe. Onesmo Buswelu akifungua kikao cha kawaida cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya SIHA mapema Leo asubuhi. Kikao hicho kinafanyika katika ukumbi wa mikutano wa HALMASHAURI ya Siha

Wajumbe wa kamati ya ushauri Wilayani SIHA wakiwa katika kikao cha kawaida cha kamati hiyo katika ukumbi wa mikutano wa HALMASHAURI ya SIHA mapema Leo asubuhi.

Tuesday 1 November 2016

Mifugo bora kwa maendeleo ya wafugaji


Moja ya mbegu bora za ng'ombe zikiwa katika malisho eneo la West KILIMANJARO hivi karibuni.

Matukio katika picha ya Kupokea mwenge wa Uhuru Wilayani Siha 2016




Wanafunzi wa shule za MSINGI NA SEKONDARI Wilayani SIHA wakiupokea na kuufurahia mwenge wa Uhuru kama alama ya Taifa la Tanzania ulipokuwa Wilayani SIHA TAREHE 28.8.2016(picha maktaba yetu)

Namna bora ya kutunza mboga za Majani katika MAENEO finyu.


Mifuko kama hii inatumika vitumike kutunzia mboga za majani kuzunguka nyumba zetu na siyo lazima kuitafuta eneo kubwa la bustani. Pia linatumika kama maua na kupitia katika makazi yetu. Hii ni tekinolojia mpya ya KILIMO iliyogundulika katika maonesho ya KILIMO nanenane mwaka huu 2016 yaliyofanyika.

Monday 31 October 2016

MPANGO WA PAMOJA TUWALEE WILAYANI SIHA



Mwenyekiti wa HALMASHAURI ya SIHA Mhe. Frank Tarimo(wa tatu kutoka kushoto) akifurahia Jambo katika shughuli za Kupokea taarifa ZA mpango wa pamoja Tuwalee zilizomaliza muda wake kwa miaka mitano katika HALMASHAURI ya Wilaya ya SIHA. Mpango huu ulikuwa NA jukumu la kuwawezesha watoto WANAOISHI katika mazingira hatarishi Wilayani SIHA NA limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Wananchi wapata elimu ya kujikinga NA ugonjwa wa TB (kifua kikuu)


Wataalam wa AFYA katika hospital ya Taifa ya kifua kikuu kibongoto Wilayani SIHA WAKITOA elimu kwa umma kwa njia ya igizo ya namna bora ya kujikinga NA ugonjwa wa TB ambao unaambukiza kwa njia ya Hewa. Igizo hilo lilifanyika mbele ya mgeni rasmi mhe. Hamis Kigwangalla Naibu waziri wa AFYA,maendeleo ya JAMII,jinsia,Wazee NA watoto alipokuwa hospitalini hapo hivi karibuni ktk zoezi la kuzindua bodi ya hospital hiyo longer hapa Nchini.

Vitalu bora vya MICHE ya miti Shamba la miti West Kilimanjaro


Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya SIHA wakiangalia jinsi wataalam wa utunzaji wa MICHE ya miti katika Shamba la miti West KILIMANJARO wanavyofanya kazi hiyo

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI SIHA WAKITOA UJUMBE KWA JAMII KWA NJIA YA NYIMBO

wanafunzi wa shule ya sekondari Sanya Juu wakitoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya nyimbo katika moja ya makongamano  yaliyofanyika Wilayani Siha hivi karibuni.

vitalu vya miche ya miti shamba la miti West KILIMANJA


MICHE YA MITI KATIKA KITALU CHA MITI WEST KILIMANJARO  INAYOSUBIRIWA KUPANDWA KATIKA MVUA ZA VULI NA MASIKA

BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU YAZINDULIWA RASMI

BAADHI YA WAJUMBE WA BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU-KIBONGOTO WAKIWA NA MGENI RASMI  MHE. HAMIS KIGWANGALLA (aliyekaa mbele wa tatu kutoka kushoto)  NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO.

SIHA YAPOKEA MADAWATI 200 KUTOKA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA KWA AJILI YA SHULE 5 ZA MSINGI

MKUU WA WILAYA YA SIHA MHE ONESMO BUSWELU (KULIA) AKIPOKEA MADAWATI 200 KUTOKA MENEJA WA SHAMBA LA MITI WEST KILIMANJARO KWA NIABA YA WAKALA WA MISITU TANZANIA
 MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL (aliyevaa shati la kitenge kushoto) AKIWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MWANGAZA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA MADAWATI 30
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NGARENAIROBI WAKIFURAHIA MADAWATI 200 YALIYOTOLEWA NA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA .MADAWATI YALITOLEWA KWA SHULE TANO ZA MSINGI WILAYANI SIHA. NGARENAIROBI MADAWATI 50,LEMOSHO MADAWATI 50,ROSELINE MADAWATI 40,NAMWAI MADAWATI 30,MWANGAZA MADAWATI 30

BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONGOTO YAZINDULIWA RASMI

MHE. HAMIS KIGWANGALLA NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AZINDUA BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONGOTO.TUKIO HILO LIMEFANYIKA MWISHONI MWA WIKI
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL AKIMPOKEA  NA KUMKARIBISHA NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO MHE. HAMIS KIGWANGALLA ALIPOTEMBELEA WILAYA YA SIHA HIVI KARIBUNI

MHE HAMIS KIGWANGALLA (KULIA) NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AKIFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA SIHA

MHE. HAMIS KIGWANGALLA  NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO AKIPOKELEWA  KATIKA WILAYA YA SIHA


MHE HAMIS KIGWANGALLA (kulia) AKITOA MAELEKEZO YA KAZI ALIPOFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU KATIKA HOSPITAL MPYA YA WILAYA YA SIHA MWISHONI MWA WIKI

WADAU WACHANGIA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI WILAYANI SIHA-PICHA

DIWANI WA KATA YA GARARAGUA MHE. ZACHARIA LUKUMAY AKITOA NENO WAKATI WA HARAMBEE YA KUKUSANYA FEDHA ZA KUKARABATI  MIUNDOMBINU CHAKAVU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SIHA VALERIAN JUWAL AKITOA MAELEKEZO YA SERIKALI ALIPOKUWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI WILAYANI SIHA

WAJUMBE WA BODI NA VINGOZI WENGINE WA SERIKALI WALIPOKUWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA  UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI HIVI KARIBUNI

MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI FELISTA KILEO AKIVALISHWA VAZI LA KIMAASAI  NA WANAFUNZI WA SHULE HIYO KAMA ISHARA YA KUPEWA ZAWADI NA BODI YA SHULE HIYO KWA KUANDAA HARAMBEE HIYO VIZURI NA UONGOZI MZURI

Thursday 27 October 2016

HABARI KATIKA PICHA

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu(aliyesimama) akitoa shukrani kwa waratibu wa mpango wa Pamoja Tuwalee kwa kuonesha na kufanikisha mpango huo kufanya vizuri ndani ya Wilaya ya Siha. shughuli hiyo ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha(picha Maktaba yetu)
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL AKITOA NENO KATIKA KILELE CHA KUFUNGA MPANGO WA PAMOJA TUWALEE ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA SIHA HIVI KARIBUNI
VIONGOZI MBALIMBALI WA WILAYA NA HALMASHAURI YA SIHA SIKU YA KUFUNGA MPANGO  WA PAMOJA TUWALEE ULIODUMU WILAYA YA SIHA KWA MUDA WA MIAKA MITANO. MPANGO HUU ULIKUWA UNASAIDIA KUWAWEZESHA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI CHINI YA UFADHILI WA WATU WA MAREKANI