Tuesday 4 July 2017

Mwenge wa Uhuru kupokelewa Siha tarehe 15.09.2017





Mwenge wa uhuru utapokelewa katika mkoa wa Kilimanjaro kupitia wilaya ya Siha tarehe 15.09.2017 ukitokea katika mkoa wa Manyara.
Hayo yamesemwa leo tarehe 04.09.2017 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Siha   na Mwenyekiti wa kamati ya sherehe za mbio za Mwenge 2017 Wilaya ya Siha ambaye pia ni mkuu wa Wilaya  Mhe.Onesmo Buswelu.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Siha aliwataka wajumbe walioshiriki katika kikao hicho kujiandaa vema katika maandalizi kabambe   ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Kilimanjaro  utapokelewa katika Wilaya ya Siha.
Mkuu wa wilaya ya siha ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama aliwaeleza wajumbe kuwa mwaka jana Siha ilifanya vizuri na kufanikiwa kushika nafasi ya Nne kati ya Wilaya  6  za mkoa wa Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa sherehe za mbio za Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Siha amewataka wananchi wa Siha kushiriki vema katika kuupokea mwenge wa uhuru wilaya siha pindi utakapowasili kwani mwenge ni mojawapo ya alama za taifa la Tanzania.
alieleza kuwa Mwenge unayo majukumu makubwa katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na kutumisha upendo,amani,utulivu na umoja miongoni mwa watanzania.
 Mwenge wa Uhuru utapokelewa Wilaya ya siha katika kijiji cha Ormelili karibu na kituo cha mabasi cha KIA na baadaye mwenge wa uhuru  utaweka mawe ya msingi,kufungua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ujumbe wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2017 ni SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU.


No comments:

Post a Comment