Sunday 29 October 2017

Kata 3 bora, Kata 3 duni matokeo Darasa la Saba 2017- Siha

Kata 3 bora matokeo Darasa la Saba 2017 -Siha

  1. MITIMIREFU
  2. LEVISHI
  3. KIRUA
Kata 3 duni matokeo Darasa la Saba 2017 -Siha
  1. DONYOMURWAK 
  2. BIRIRI
  3. NDUMET

Thursday 26 October 2017

Shule 10 bora na shule 10 duni matokeo darasa la Saba 2017 Wilaya ya Siha

Shule 10 Bora matokeo darasa la Saba  2017 -SIHA
  1. PUNCHMI
  2. SAMAKI
  3. NGARONY
  4. NKYARE
  5. GARARAGUA
  6. NURU
  7. KYENGIA
  8. FUKA ENG MED
  9. LOKIRI
  10. FUKA
Shule 10 duni matokeo darasa la Saba 2017-SIHA
  1. KIRISHA
  2. SABUKU
  3. KANDASHI
  4. DONYOMURWA
  5. ROSELINE
  6. SANYA JUU
  7. MAKIWARU
  8. KISHISHA
  9. NAIBILI
  10. EMBUKOI



Wanawake Wapatiwa Mikopo




Vikundi 22 Wanawake vyapatiwa mikopo  2016/2017

Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imefanikiwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi 22 vya wanawake Wilayani Siha katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal alieleza hayo katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Taarifa ya Mkurugenzi mtendaji ilieleza kuwa,katika mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri ya Wilaya ya Siha imetoa mikopo kwa vikundi  22 vya wanawake Wilayani Siha yenye thamani ya shilingi 56 ,000,000/= zikiwa ni fedha kutoka mchango wa Halmashauri wa asilimia tano (5%) ya mapato yake ya  ndani.

Aidha, Mkurugenzi katika taarifa yake alieleza Baraza kuwa pamoja na changamoto ya halmashauri kukabiliwa na vyanzo vichache vya ukusanyaji wa mapato lakini Halmashauri imejitahidi kutoa kiasi hicho cha fedha kwa vikundi vilivyoomba mikopo na vilivyotimiza vigezo vya kupata mikopo hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu mbalimbali.

Ametoa wito kwa vikundi vya wanawake katika wilaya ya Siha kutumia fursa hiyo ya Serikali  ya kuomba mikopo yenye masharti nafuu  katika kujikwamua kiuchumi katika ngazi ya Familia na jamii kwa ujumla wake.

Hata hivyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ametoa wito kwa vikundi  mbalimbali vilivyopatiwa mikopo kutumia mikopo hiyo kwa shughuli waliojipangia  badala ya kutumia mikopo waliyopewa  katika mambo yasiyoleta tija.
Alieleza kuwa pamoja na jitihada za halmashauri kutoa mikopo hiyo kwa wanawake  lakini wahusika bado wanayo wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati ili iweze kuwasaidia wanufaika wengine katika halmashauri ya Wilaya ya Siha.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha katika upangaji wa mipango na bajeti kila mwaka inatenga asilimia 5 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha wanawake na asilimia 5 ya mapato ya ndani ya Halmashauri  mikopo kwa vikundi vya vijana.


Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ilitenga bajeti ya Tsh 87,051,850 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake. Ambapo hadi kufikia Juni 2017 jumla ya vikundi ishirini na mbili (22) vya wanawake vilipatiwa mkopo wenye thamani ya Tshs 56,000,000/= zikiwa ni fedha kutoka mchango wa Halmashauri wa asilimia tano (5%) ya mapato ya ndani.

Wednesday 25 October 2017

Siha yafanikiwa zoezi la utoaji wa chanjo mwaka 2016/2017




Utoaji wa Chanjo Wafanikiwa  Wilaya ya Siha mwaka 2016/2017
Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imefikia zaidi ya asimia 96 ya huduma  ya utoaji wa chanjo mbalimbali ya kujikinga na magonjwa kwa watoto Wilayani hapa.

Katika taarifa ya mwaka 2016/2017 iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha  Valerian Juwal katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani lililokutana mwezi Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji ilieleza kuwa katika huduma ya utoaji wa chanjo mbalimbali kwa watoto, halmashauri ya Wilaya ya Siha imefanikiwa kutoa chanjo ya matone ya vitamin A na dawa za minyoo hadi kufikia asilimia 96.7

Aidha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji ilieleza kuwa,katika huduma ya utoaji wa chanjo ya kansa ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wenye umri  chini ya miaka 14,zoezi hilo pia  lilifanikiwa kwa  zaidi ya asilimia 87.

Mkurugenzi Mtendaji alieleza  Baraza la Madiwani kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Siha ni  miongoni mwa Halmashauri za Wilaya hapa nchini zilizofanya vizuri katika usimamiaji wa zoezi zima la utoaji chanjo kwa watoto.

Alieleza kuwa siri ya mafanikio  ya zoezi hilo ni ushirikiana wa dhati  baina ya Wananchi ,viongozi na wadau wengine wa maendeleo katika Wilaya ya Siha.

Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Siha aliwaomba wananchi na viongozi wa Siha kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuboresha afya ya wananchi wake hasa utoaji wa chanjo unaosaidia kutoa kinga mbalimbali kwa watoto.

Vile vile,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha alieleza Baraza la Madiwani kuwa huduma ya chanjo zote alizozitaja hutolewa bure kwa kugharamiwa na Serikali na hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa mara moja iwapo watatokea watu wanaowadai fedha za kulipia huduma hiyo.


Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012 Halmashauri ya Wilaya ya Siha inajumla ya watu 116,313 wakiwemo wanaume 56,500 na wanawake 59,813.


Monday 23 October 2017

Picha matukio zoezi la usaili ajira mpya halmashauri ya Siha Oktoba 23,2017




walioitwa katika usaili ajira mpya halmashauri ya Siha wakiwa katika majengo ya shule ya Sekondari Kilingi wakisubir maelekezo ya usaili mapema leo asubuhi tarehe


 walioitwa katika usaili Halmashauri ya Siha wakifanya usaili wa maandishi katika moja ya vyumba vilivyoandaliwa na Halmashauri ya Siha

  mafuriko ya walioitwa katika usaili wakisikiliza maelekezo  kutoka kwa Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Siha mara baada ya kutoka katika usaili


 Hawa ni baadhi  tu ya walioitwa katika usaili katika halmashauri ya Siha wakiwa katika shule ya Sekondari Kilingi
 Afisa utumishi na Utawala Nico Kayange katikati akitoa maelekezo mbalimbali kwa waliomba ajira mpya Siha

Usaili ukifanyika chini ya uangalizi makini wa Maofisa wa Halmashauri ya Siha waliokabidhiwa jukumu hilo .zoezi hilo zimeanza leo kwa mchujo wa kwanza na litaendelea hadi tarehe 25.10.2017