Monday 31 October 2016

MPANGO WA PAMOJA TUWALEE WILAYANI SIHA



Mwenyekiti wa HALMASHAURI ya SIHA Mhe. Frank Tarimo(wa tatu kutoka kushoto) akifurahia Jambo katika shughuli za Kupokea taarifa ZA mpango wa pamoja Tuwalee zilizomaliza muda wake kwa miaka mitano katika HALMASHAURI ya Wilaya ya SIHA. Mpango huu ulikuwa NA jukumu la kuwawezesha watoto WANAOISHI katika mazingira hatarishi Wilayani SIHA NA limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Wananchi wapata elimu ya kujikinga NA ugonjwa wa TB (kifua kikuu)


Wataalam wa AFYA katika hospital ya Taifa ya kifua kikuu kibongoto Wilayani SIHA WAKITOA elimu kwa umma kwa njia ya igizo ya namna bora ya kujikinga NA ugonjwa wa TB ambao unaambukiza kwa njia ya Hewa. Igizo hilo lilifanyika mbele ya mgeni rasmi mhe. Hamis Kigwangalla Naibu waziri wa AFYA,maendeleo ya JAMII,jinsia,Wazee NA watoto alipokuwa hospitalini hapo hivi karibuni ktk zoezi la kuzindua bodi ya hospital hiyo longer hapa Nchini.

Vitalu bora vya MICHE ya miti Shamba la miti West Kilimanjaro


Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya SIHA wakiangalia jinsi wataalam wa utunzaji wa MICHE ya miti katika Shamba la miti West KILIMANJARO wanavyofanya kazi hiyo

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI SIHA WAKITOA UJUMBE KWA JAMII KWA NJIA YA NYIMBO

wanafunzi wa shule ya sekondari Sanya Juu wakitoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya nyimbo katika moja ya makongamano  yaliyofanyika Wilayani Siha hivi karibuni.

vitalu vya miche ya miti shamba la miti West KILIMANJA


MICHE YA MITI KATIKA KITALU CHA MITI WEST KILIMANJARO  INAYOSUBIRIWA KUPANDWA KATIKA MVUA ZA VULI NA MASIKA

BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU YAZINDULIWA RASMI

BAADHI YA WAJUMBE WA BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU-KIBONGOTO WAKIWA NA MGENI RASMI  MHE. HAMIS KIGWANGALLA (aliyekaa mbele wa tatu kutoka kushoto)  NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO.

SIHA YAPOKEA MADAWATI 200 KUTOKA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA KWA AJILI YA SHULE 5 ZA MSINGI

MKUU WA WILAYA YA SIHA MHE ONESMO BUSWELU (KULIA) AKIPOKEA MADAWATI 200 KUTOKA MENEJA WA SHAMBA LA MITI WEST KILIMANJARO KWA NIABA YA WAKALA WA MISITU TANZANIA
 MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL (aliyevaa shati la kitenge kushoto) AKIWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MWANGAZA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA MADAWATI 30
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NGARENAIROBI WAKIFURAHIA MADAWATI 200 YALIYOTOLEWA NA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA .MADAWATI YALITOLEWA KWA SHULE TANO ZA MSINGI WILAYANI SIHA. NGARENAIROBI MADAWATI 50,LEMOSHO MADAWATI 50,ROSELINE MADAWATI 40,NAMWAI MADAWATI 30,MWANGAZA MADAWATI 30

BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONGOTO YAZINDULIWA RASMI

MHE. HAMIS KIGWANGALLA NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AZINDUA BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONGOTO.TUKIO HILO LIMEFANYIKA MWISHONI MWA WIKI
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL AKIMPOKEA  NA KUMKARIBISHA NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO MHE. HAMIS KIGWANGALLA ALIPOTEMBELEA WILAYA YA SIHA HIVI KARIBUNI

MHE HAMIS KIGWANGALLA (KULIA) NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AKIFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA SIHA

MHE. HAMIS KIGWANGALLA  NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO AKIPOKELEWA  KATIKA WILAYA YA SIHA


MHE HAMIS KIGWANGALLA (kulia) AKITOA MAELEKEZO YA KAZI ALIPOFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU KATIKA HOSPITAL MPYA YA WILAYA YA SIHA MWISHONI MWA WIKI

WADAU WACHANGIA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI WILAYANI SIHA-PICHA

DIWANI WA KATA YA GARARAGUA MHE. ZACHARIA LUKUMAY AKITOA NENO WAKATI WA HARAMBEE YA KUKUSANYA FEDHA ZA KUKARABATI  MIUNDOMBINU CHAKAVU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SIHA VALERIAN JUWAL AKITOA MAELEKEZO YA SERIKALI ALIPOKUWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI WILAYANI SIHA

WAJUMBE WA BODI NA VINGOZI WENGINE WA SERIKALI WALIPOKUWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA  UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI HIVI KARIBUNI

MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI FELISTA KILEO AKIVALISHWA VAZI LA KIMAASAI  NA WANAFUNZI WA SHULE HIYO KAMA ISHARA YA KUPEWA ZAWADI NA BODI YA SHULE HIYO KWA KUANDAA HARAMBEE HIYO VIZURI NA UONGOZI MZURI

Thursday 27 October 2016

HABARI KATIKA PICHA

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu(aliyesimama) akitoa shukrani kwa waratibu wa mpango wa Pamoja Tuwalee kwa kuonesha na kufanikisha mpango huo kufanya vizuri ndani ya Wilaya ya Siha. shughuli hiyo ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha(picha Maktaba yetu)
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL AKITOA NENO KATIKA KILELE CHA KUFUNGA MPANGO WA PAMOJA TUWALEE ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA SIHA HIVI KARIBUNI
VIONGOZI MBALIMBALI WA WILAYA NA HALMASHAURI YA SIHA SIKU YA KUFUNGA MPANGO  WA PAMOJA TUWALEE ULIODUMU WILAYA YA SIHA KWA MUDA WA MIAKA MITANO. MPANGO HUU ULIKUWA UNASAIDIA KUWAWEZESHA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI CHINI YA UFADHILI WA WATU WA MAREKANI

MATUKIO KATIKA PICHA

 sehemu ya bustani ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha -Kilimanjaro katika maonesho ya kilimo nanenane Arusha kwa mwaka huu 2016(picha Maktaba )
muonekano wa  banda la Halmashauri ya Wilaya ya Siha -Kilimanjaro katika maonesho ya kilimo nanenane Arusha  kwa mwaka 2016 (picha maktaba)
 Hawa ni baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro wakiwa katika mazoezi ya kawaida kwa ajili ya kuboresha afya zao(picha maktaba yetu)
 mchezo wa magunia ni miongoni mwa michezo isiyopewa kipau mbele hapa nchini na Duniani lkn kwa upande wa watumishi wa Halmashauri ya Siha wameamua kuundeleza mchezo huu. picha ya bonanza la michezo mwishoni mwa mwaka jana(picha maktaba yetu)
watumishi wa halmashauri ya Siha wakiwa katika maandalizi ya kufanya mazoezi ya kukimbia kwa gunia kwa upande wa wanaume(picha ya maktaba)

Monday 24 October 2016

WADAU WACHANGIA ELIMU WILAYANI SIHA-KILIMANJARO





Wadau wachangia elimu shule ya sekondari Magadini

Wadau mbalimbali wa elimu Wilayani Siha wamechangia fedha za ukarabati wa miundombinu ya shule ya Sekondari Magadini iliyopo Kata ya Gararagua Wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro.

Harambee hiyo iliandaliwa na Bodi ya Shule ya Sekondari Magadini kwa ushirikiano na Uongozi wa Shule  hiyo pamoja na uongozi wa Kata  na Vijiji. 

Katika harambee hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Shule ya Sekondari Magadini zaidi ya Tsh. Milioni 5 zilikusanywa, fedha hizi  zinajumuisha fedha taslimu,ahadi na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa  na wadau .

Awali akitoa taarifa  fupi kwa mgeni rasmi katika harambee hiyo mkuu wa shule Felista Kileo  alieleza kuwa wameona ni vema kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo ili kuboresha  mazingira ya kujifunza na kufundishia.

Alieleza kuwa fedha na vifaa mbalimbali vilivyopatikana vitasaidia katika kuboresha na kukarabati madarasa kachakavu katika shule hiyo yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.

Katika harambee hiyo ,Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu alichangia mifuko 35 ya saruji yenye thamani ya shilingi 525,000/= ambapo mchango wake ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Siha.

Monday 17 October 2016

UFUGAJI WA NYUKI WASAIDIA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KIJIJI CHA MATADI- WEST KILIMANJARO

 BAADHI YA WAFUGAJI NYUKI KIJIJI CHA MATADI WAKITUNDIKA MIZINGA YA NYUKI KATIKA MAENEO YALIYOTUNZWA MAZINGIRA VIZURI
WAFUGAJI WA NYUKI WAKIPATA ASALI MARA BAADA YA ZOEZI LA URINAJI WA ASALI KUFANYIKA.
 WANANCHI WA KIJIJI CHA MATADI WAKIFURAHIA UTUNZAJI MZURI WA MAZINGIRA ULIVYOSAIDIA ONGEZEKO LA UPATIKANAJI WA ZAO LA ASALI KATIKA KIJIJI CHAO

WAFUGAJI WA NYUKI KIJIJI CHA MANIO WAPATIWA MIZINGA YA KISASA ZAIDI YA 40

DIWANI WA KATA YA KASHASHI MHE. SUZAN NATAI AKIPOKEA MIZINGA YA KISASA ZAIDI YA AROBAINI KWA AJILI YA WANANCHI WAKE WA KIJIJI CHA MANIO
DIWANI WA KATA YA KASHASHI SUZAN NATAI AKISHUKURU HALMASHAURI YA SIHA  KWA KUWAPATIA WAFUGAJI WA NYUKI KTK KIJIJI CHAKE MIZINGA YA KISASA
MWAKILISHI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SIHA DR BARNABAS MBWAMBO AKITUNDIKA MIZINGA KATIKA KIJIJI CHA MANIO KATA YA KASHASHI
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA UFUGAJI NYUKI ERNEST MARANDU AKITOA MAELEZO YA MATUMIZI YA MIZINGA ILIYOKABIDHIWA NA HALMASHAURI YA SIHA KWA WAFUGAJI WA KIJIJI CHA MANIO KATA YA KASHASHI
MIZINGA ILIYOTUNDIKWA NA WAFUGAJI WA NYUKI KIJIJI CHA MANIO  MARA BAADA YA KUKABIDHIWA

UTUNZAJI WA MAZINGIRA KIJIJI CHA MANIO- WILAYANI SIHA WASAIDIA WAFUGAJI WA NYUKI

Mizinga zaidi ya arobaini yakabidhiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Siha  kwa Wafugaji wa nyuki  Kijiji cha MANIO Kata ya KASHASHI WILAYA YA SIHA MKOA WA KILIMANJARO. Kata ya Kashashi pia ipo katika mpango wa utunzaji wa matumizi endelevu ya ardhi
mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha Dr. Barnabas Mbwambo akishirikiana na Wananchi wa Kijiji cha Manio  Kata ya Kashashi katika  zoezi la utundikaji wa mizinga ya kisasa. zoezi hilo limefanyika hivi karibuni 
baadhi ya wafugaji wa Kijiji cha Manio wakisubiri kukabidhiwa mizinga katika kijiji chao
Diwani wa Kata ya Kashashi Mhe. Suzan Natai (wa tatu kutoka kulia) akipata maelezo ya kitaalamu baada  ya zoezi la kukabidhiwa mizinga ya nyuki kwa wafugaji wa kijiji cha Manio.

UTENZI WA KUMUENZI BABA WA TAIFA MWL JULIUS K NYERERE











UTENZI WA KUMUENZI HAYATI BABA  WA TAIFA MWL JULIUS K NYERERE 14/10/2016

1. Naanza kwa kumsifu,
Mungu wetu Mtukufu,
Yeye ni fundi Sanifu,
Sisi tumeumbwa naye.

2. Namtaja wetu Mungu,
Aliyekuwe tangu ,
Amezitundika Mbingu,
Ardhi katugawia.

3. Kwake yeye tunaishi,
Sisi kwake watumishi,
Wala hakuna ubishi,
Pumzi katujalia.

4. Mungu huyu ana utu,
Anazo nafsi tatu,
Roho,mwana,baba yetu,
Mola mmoja sikia.

5. Huyu ni wetu mkubwa,
Anayetoa ubwabwa,
Siriye imesiribwa,
Hakuna wa kufasiri.

6. Ba’da ya kumshukuru,
Mungu bila ya kukufuru,
Sasa ninayanukuru,
Niliyoyakusudia.

7. Nianze kusimulia,
Tendo la kihistoria,
Kifupi nitayasogoa,
Sikilizeni kwa makini.

8. Kwanza twarejea nyuma,
Kwa makini kutozama,
Tulivyofanywa wanyama,
Katika yetu aridhi.

9. Mkoloni kang’ang’ania,
Nchi akaikalia,
Wakaumia raia,
Wasijue la kufanya.

10. Akatokea kijana,
Mwenye upeo mpana,
Kasema tutapambana,
Tanganyika tuwe huru.

11. Namtaja Juliasi,
Huyu ndiye muasisi,
Kasema siyo rahisi,
Lakini tutaupata.

12. Mkoloni kakasirika,
Akaitwa kibaraka,
Mroho wa madaraka,
Tena asiyetosheka.

13. Wakoloni wauaji,
Ni wakubwa wanyonyaji,
Baba kawavua taji,
Uhuru tukaupata.

14. Tarehe tisa disemba,
Wananchi tukaimba,
Tukacheza na sindimba,
Uhuru kushangilia.

15. Falsafa ya ujamaa,
Ndiyo ilikuwa taa,
Pia kujitegemea,
Iwe ndio yetu njia.

16. Lugha yetu Kiswahili,
Ni mkubwa mhimili,
Juliasi kakubali,
Iunganishe raia.

17. Ni mwana diplomasia,
Mpenda Demokrasia,
Haki zote za raia,
Yeye aliyepigania.

18. Usawa wa Binadamu,
Kaka dada na binadamu,
Sote tushike hatamu,
Kuleta maendeleo

19. Na elimu ya Msingi,
Aliyesema mambo mengi,
Isiwekewe vigingi,
Ni haki  ya kila mtu.

20. Nchi zote kapitia,
Afrika nzimasikia,
Hamasa akiwatia,
Lazima wajitawale.

21. Kasema Afrika viva,
Kongo mambo yakaiva,
Msumbiji,Angola viva,
Zimbabwe na Namibia.

22. Pote aliheshimika,
Wakawa na uhakika,
Bendera wakasimama,
Hongera baba Nyerere.

23. Jama huu ni utenzi,
Una nyingi sana beti,
Ninalikunja busati,
Wengine wamalizie,

24. Mengi nimeelezea,
Kuwachosha siyo nia,
Kwa hapa nitakomea,
Hadi wakati mwingine.

Imeandaliwa na kusomwa na:
MWL JUSTINA MOHAMED NGOLINDA
SHULE YA Sekondari Oshara-SIHA KILIMANJARO

PICHA ZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA WILAYANI SIHA

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya kumbukumbu ya baba wa Taifa mwl Julius K Nyerere. Maadhimisho hayo yalifanyika katika uwanja wa CCM Sanya Juu tarehe 14.10.2016
Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maadhimiro ya miaka 17 ya kumkumbuka baba wa taifa mwl Julius K Nyerere. Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza fedha zote za posho zilizokuwa zimetolewa kwa watumishi wa ofisi yake na ile ya Mkurugenzi wa Halmashauri ikiwa ni pamoja na za maandalizi ya mwenge zilizokuwa zimetengwa kwa mwaka huu 2016/2017 zielekezwe kununulia madawa hospital ya Wilaya na kuboresha miundombinu Zahanati ya Ormelil.
Mmoja wa watoa mada Katika maadhimisho ya baba wa Taifa Wilayani Siha (Mwl Ngolinda wa Shule ya Sekondari Oshara) akitoa mada namna anavyomfahamu baba wa Taifa    
MKURUGENZI MTENDAJI H/W SIHA VALERIAN JUWAL (anayeshangilia kwa makofi) akifurahia maonesho yaliyokuwa yakifanywa na watoto wa Halaiki katika uwanja wa mpira wa miguu  Sanya juu. maadhimisho hayo yaliongozwa na mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu(aliyevaa suti nyeusi mbele ya Bendera)
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Sanya Juu wakitumbuiza katika maadhimisho ya kumkumbuka ya Baba wa Taifa Wilaya ya Siha.
Wanafunzi wa  Halaiki Wilayani Siha wakitoa ujumbe wa mshikamano na upendo kama ishara ya kumkumbuka baba wa Taifa Mwl Julius K Nyerere.
mmoja wa washiriki (Mzee Daniel Sandewa)  kwa niaba ya wazee wa Siha akitoa neno la Shukurani kwa Wananchi wa Siha kwa namna walivyoshiriki vema katika kumkumbuka baba wa Taifa la Tanzania