Tuesday 11 July 2017

Kaya 1,871 wanufaika na mpango wa TASAF kwa mwaka 2016/2017




Mpango wa Serikali wa kunusuru kaya maskini Wilaya ya Siha umewanufaisha  kaya 1,871 zilizopo katika vijiji 24 Wilayani hapa.

Halmashauri ya Wilaya  ya Siha kwa kutumia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kipindi  cha Julai 2016 hadi Juni, 2017 imeweza kuhaulisha kiasi cha Tsh.413,280,000.00 kwa lengo la kusaidia kaya maskini Wilayani hapa.

Hayo yamesemwa na Mhe  Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha katika taarifa ya wilaya ya Siha  aliyoitoa kwa Mhe Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alipofanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Siha tarehe 10.07.2017.

Taarifa hiyo pia  ilieleza kuwa fedha hizo za kunusuru kaya maskini zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuletwa moja kwa moja kwa halmashauri kwa ajili ya kupelekwa kwa wahusika ambao hupatikana kupitia taratibu zilizopangwa.

No comments:

Post a Comment