Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro itaweka kipau mbele suala la kuwawezesha walemavu wa ngozi kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal katika maazimisho ya siku ya watu wenye Ualbino yaliyofanyika Kiwilaya katika ofisi ya Kijiji cha Lawate tarehe 15.06.2017.
Katika hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Siha aliagiza idara ya maendeleo ya Jamii na ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa walemavu wa ngozi Wilayani Siha wanapewa fursa za kuwezeshwa katika mikono kama wanavyopewa makundi mengine hasa yale ya vijana na wanawake.
Alieleza kuwa fedha hizo zinaweza kutolewa katika asilimia kumi ya Mapato ya ndani ambazo kimsingi hutengwa kila mwaka kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya vijana na Kinamama.
Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa kwa nafasi yake atahakikisha kuwa jinsi hilo muhimu linapatiwa huduma zinazohitajika kama vile Elimu,afya na ulinzi wa kutosha kwa ushirikiano wa wadau wa maendeleo,wananchi na viongozi mbalimbali katika jamii.
Pia Mkurugenzi Mtendaji alitoa wito kwa jamii ya wanasiha kuendelea kushirikiana na Serikali katika suala la ulinzi na usalama kwa watu wenye Ualbino katika Wilaya ya Siha.
Maazimisho ya mwaka huu yamekuwa na kauli mbiu Umuhimu wa Takwimu na Tafiti kwa ustawi wa Watu wenye Ualbino
No comments:
Post a Comment