Mkuu wa Wilaya ya
Siha Mhe. onesmo Buswelu amepiga marufuku biashara ya uchomaji,uuzaji na
usafirishaji wa mahindi mabichi ndani na Nje ya Wilaya.
Agizo hilo
amelitoa leo tarehe 19.06.2017
alipokuwa katika ukaguzi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi inayojengwa katika
kijiji cha Sanya hoyee Kata ya Sanya Juu.
Mkuu wa Wilaya ya
Siha ameeleza kuwa sababu kubwa ya kutoa amri hiyo halali ni pamoja na
malalamiko mengi aliyoyapokea ya wizi wa mahindi mabichi mashambani kutoka kwa
viongozi wa Vijiji na Vitongoji Wilayani hapa.
Alieleza kuwa amri
hiyo inatekelezwa kuanzia leo tarehe 19.06.2017 hadi msimu wa mavuno ya
masika kwa mwaka 2017 utakapokamilika.
Mhe Onesmo Buswelu
ametoa wito kwa Wananchi wa Siha kuhakikisha wanaweka akiba na ziada ya chakula
kwa ajili ya familia zao na kuepukana na kuuza chakula chote kwa tamaa za
kujipatia fedha.
amewataka pia
Wananchi wa Wilaya ya Siha kuzingatia agizo la kutotumia nafaka ya mahindi kwa
ajili ya utengenezaji wa pombe za kienyezi na badala yake watumia nafaka
mbadala kama vile ngano na shairi kama wakiona ni lazima kufanya hivyo.
Kwa msimu wa mwaka
2017,Wilaya ya Siha inategemea kupata msimu mzuri wa chakula hasa zao la
mahindi ,viazi na ndizi.
No comments:
Post a Comment