Wilaya
ya Siha kuazimisha siku ya watu wenye Ualbino
Halmashauri ya Wilaya ya Siha
mkoa wa Kilimanjaro itaazimisha siku ya watu wenye Ualbino(Albinism) siku ya Alhamis tarehe 15
Juni,2017.
Maazimisho ya siku ya watu
wenye Ualbino Kiwilaya yanategemewa
kufanyika katika ofisi ya kijiji cha Lawate huku kauli mbiu ya mwaka 2017 ikiwa “Umuhimu wa takwimu na tafiti kwa ustawi wa watu wenye Ualbino”.
Aidha,maazimisho hayo
yatafanyika kwa mara ya kwanza Wilayani Siha kwa mwaka 2017, huku Wilaya ya
Siha ikiwa na historia nzuri ya kuwatunza na kuwalinda watu wenye Ualbino.
Hadi sasa Wilaya ya Siha haina
tukio lolote lililotokea na kuripotiwa juu ya kitendo chochote cha
kuwanyanyasa,kuwajeruhi au mauaji ya walemavu wa ngozi waliopo katika Wilaya ya
Siha.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Siha anatoa wito kwa Wananchi na Wakazi wa Wilaya ya Siha
kuendelea na moyo huo wa upendo wa kuwatunza na kuwalinda ndugu zetu wenye
Ualbino hasa kwa kuwapatia mahitaji yao muhimu kama elimu,huduma za Afya na
huduma nyingine muhimu.
Wilaya ya Siha inakadiriwa kuwa
na watu wenye Ualbino wapatao 11 ambao wanaishi na jamii katika maeneo tofauti
tofauti Wilayani hapa.
No comments:
Post a Comment