Monday, 10 October 2016

WILAYA YA SIHA-KILIMANJARO VINARA KUWAJALI WATOTO


Halmashauri ya Wilaya ya Siha imepongezwa kwa kuwa Halmashauri ya kwanza kanda ya Kaskazini kati ya Halmashauri 17 zilizokuwa katika mpango wa kuwasaidia na kuwanusuru watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kupambana na tabia ya ukeketaji wa wanawake.

hayo yamesemwa na Grace Muro  Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali linalojulikana kama  Pamoja  Tuwalee ambalo linadhaminiwa na Watu wa Marekani. aliyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha wakati shirika hilo likiwa katika mkutano wa kufunga mradi wa makabidhiano wa mpango huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha.

Mwakilishi huyo alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha imekuwa mfano wa kuigwamiongoni mwa Halmashauri 17 mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambapo mpango huo uliendeshwa tangu mwaka 2010.

aidha ,aliendelea kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha imekuwa ikiweka fedha za kutoshakatika bajeti zake za kila mwaka ambazo zimeweza kufanikisha kusaidia watoto wanaishi mazingira magumu kupata misaada ya chakula,elimu,afya na huduma za kisaikolojia.

alieleza kuwa katika Wilaya ya Siha jumla ya watoto 5370 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita  wamepatika huduma mbalimbali na Mpango unadhamini na Shirika la Pamoja Tuwalee. miongoni mwa huduma walizopatiwa ni pamoja na huduma za vifaa vya Elimu,ulinzi nausalama kwa watoto,lishe bora kwa watoto,huduma za kuwezeshwa kiuchumi,pamoja na huduma za kisaikolojia.

mwakilishi huyo alitoa wito kwa Halmashauri zote Nchini kutenga bajeti za kutosha kila mwaka kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwani idadi yao inazidi kuongezeka kila mwaka.

Alieleza kuwa jamii kwa upande mwingine inatakiwa kuelimishwa na kutambua kuwa inaowajibu wa kuwahudumia watoto hao kwani watoto hao hawakuzaliwa na mitaa wala vijiji bali wamezaliwa na binadamu wenzetu ambao kwa bahati mbaya wamepata matatizo tofauti ya kifamilia.

Mgeni rasmi katika mkutano wa kufunga mradi huo Mheshimiwa Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha alianza kwa kuwashukuru shirika la Pamoja tuwalee kwa namna ya kipekee walivyoweza kushirikiana na Wilaya ya Siha katika majukumu ya kuwapatia mahitaji watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

alieleza kuwa pamoja na mradi huo kufika ukomo katika Wilaya ya Siha baada ya kumaliza muda wake  lakini aliwaomba wahisani hao kufikiria namna ya kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kutafuta misaada mbalimbali ya kuwasaidia watoto hao kwani mahitaji bado ni makubwa sana.

aliitaka Halmashauri ya Siha kutobweteka kwa kupewa sifa nyingi za kuongoza na kufanya vizuri katika kutoa huduma za watoto badala yake wachukulie kama ni changamoto ya kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wahitaji ambao ni watoto.


No comments:

Post a Comment