Wadau wachangia elimu
shule ya sekondari Magadini
Wadau mbalimbali wa elimu Wilayani Siha wamechangia fedha za
ukarabati wa miundombinu ya shule ya Sekondari Magadini iliyopo Kata ya
Gararagua Wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro.
Harambee hiyo iliandaliwa na Bodi ya Shule ya Sekondari
Magadini kwa ushirikiano na Uongozi wa Shule hiyo pamoja na uongozi wa Kata na Vijiji.
Katika harambee hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
Shule ya Sekondari Magadini zaidi ya Tsh. Milioni 5 zilikusanywa, fedha
hizi zinajumuisha fedha taslimu,ahadi na
vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wadau .
Awali akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi katika harambee hiyo mkuu
wa shule Felista Kileo alieleza kuwa
wameona ni vema kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuunga mkono
jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha miundombinu ya shule
hiyo ili kuboresha mazingira ya
kujifunza na kufundishia.
Alieleza kuwa fedha na vifaa mbalimbali vilivyopatikana
vitasaidia katika kuboresha na kukarabati madarasa kachakavu katika shule hiyo
yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.
Katika harambee hiyo ,Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo
Buswelu alichangia mifuko 35 ya saruji yenye thamani ya shilingi 525,000/=
ambapo mchango wake ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Siha.
No comments:
Post a Comment