Wednesday, 24 May 2017

TAARIFA KWA UMMA



OFISI YA RAIS TAMISEMI
                             HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

   
TAARIFA KWA UMMA 

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro inapenda kuujulisha Umma kuwa taarifa iliyotolewa na gazeti la Nipashe la tarehe 23 Mei,2017 yenye kichwa cha maneno “Viwanja Vyageuzwa Mashamba Kodi”
 
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Siha inapenda kuufahamisha Umma kuwa taarifa iliyotolewa siyo sahihi na ilikuwa na lengo la kuupotosha Umma na kuwapa hofu wanaomiliki viwanja Siha. Ukweli wa jambo hili ni kuwa eneo lililokodishwa na Halmashauri  lenye ukubwa wa hekari 767 siyo eneo la  viwanja kama ilivyoandikwa na gazeti tajwa hapo juu, bali eneo hili lilitengwa na Halmashauri ya Siha kwa ajili ya shughuli za uwekezaji. 

Aidha,Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Siha inapenda kufahamisha Wananchi wote wanaomiliki viwanja vilivyopimwa  katika Halmashauri ya Siha kuwa viwanja vyao vipo salama na Halmashauri haijawahi kubadilisha matumizi ya ardhi hiyo.

Hata hivyo,Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Siha inatoa wito kwa Wananchi wote wanaomiliki viwanja katika eneo la Halmashauri kuviendeleza viwanja wanavyomiliki.

 Imetolewa na:-

Zakayo Elifaison
Mkuu wa Kitengo cha Habari & Mawasiliano Halmashauri (W) Siha
24 Mei, 2017









Milioni 36 kutolewa kwa Wanawake Siha



Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kutoa zaidi ya Shilingi milioni 36 kwa ajili ya mikopo ya Wanawake Wilayani hapa.

Jumla ya vikundi 12 vyenye wanufaika 249 vinatarajiwa kufaidika  na fedha hizo zinazotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Siha. Fedha zinazotolewa  na Halmashauri ya Wilaya ya Siha  ni sehemu ya ya  asilimia 5 ya  Mapato ya ndani  ya Halmashauri.

Mwezi Agosti katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 Halmashauri ya Wilaya ya Siha ilitoa Mikopo kwa vikundi 10 vya Wanawake Wilayani Siha vilivyokuwa na wanufaika 157 yenye thamani ya Shilingi milioni 20 ambapo kila kikundi kilipatiwa mkopo wa Shilingi milioni mbili.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha katika utekelezaji wa bajeti yake kila mwaka  imekuwa ikitenga asilimia 5 ya Mapato ya ndani kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake na asilimia 5 kwa ajili ya Vijana.

Friday, 19 May 2017

Madiwani wa Halmashauri ya Siha wafanya mkutano wa Kawaida wa Baraza hilo.

 Mkutano wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Wilaya ya Siha wakutana kwa siku mbili tarehe 18.5.2017 na 19.5.2017. Mkutano huo umefayika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Siha na kujadili na kupitia taarifa mbalimbali ya shughuli zilizotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2016/2017.
Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Siha wakiwa katika mkutano  wa Kawaida wa Baraza katika ukumbi wa Mikutano wa Baraza hilo.

Wednesday, 17 May 2017

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule asema maendeleo hayana Itikadi

WANANCHI SIHA WATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA

DC SIHA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA sERIKALI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

 Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe Onesmo Buswelu akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari Fuka tarehe 16.5.2017
 Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe Onesmo Buswelu akikagua ujenzi wa Choo cha Shule ya Msingi Lomakaa kata ya Kirua
 Mkuu wa Wilaya ya Siha akiongea na Wazazi na Wananchi wa Kata ya Kirua katika shule ya Sekondari Fuka tarehe 16.5.2017

Tuesday, 16 May 2017

Siha Yahitaji Walimu 54 wa Masomo ya Sayansi,Hisabati



Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro inahitaji walimu 54 wa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa shule za Sekondari za Serikali.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya shule kwa Mkuu wa Wilaya ya Siha,Mkuu wa shule ya Sekondari Fuka  Mwalimu Swalehe Kombo alieleza kuwa Shule yake inahitaji kubwa la walimu wa Sayansi na hasa kwa somo la  Hisabati.

Mkuu huyo wa Shule aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Halmashauri ya Wilaya ya  Siha  kwa kuwapatia mwalimu mmoja wa somo la Biolojia na Jiografia katika ajira mpya zilizotolewa na Serikali  hivi karibuni. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal alieleza kuwa  Wilaya ya Siha ilipata Walimu watatu wa masomo ya Sayansi katika ajira mpya zilizotangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni.

Alisema kuwa kati ya Walimu watatu wa masomo ya Sayansi na Hisabati waliopangwa Wilaya ya Siha mwalimu mmoja alipangwa shule ya Sekondar Fuka na wengine katika shule ya Sekondari Sanya Juu na shule ya Sekondari Nuru.

Hata hivyo alieleza kuwa Serikali bado itaendelea kuajiri Walimu wa masomo ya Sayansi kwa shule za Msingi na Sekondari kwani mahitaji bado ni makubwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha aliwataka Wananchi  na wadau wa maendeleo kuendelea kukamilisha ujenzi wa maabara kwani ndiyo suluhisho la pekee litakalosaidia kupatikana kwa wataalam wa Sayansi na Hisabati.

Wilaya ya Siha inahitaji jumla ya Walimu 54 wa Masomo ya Sayansi na Hisabati kwa shule za Sekondari za Serikali.