Tuesday, 16 May 2017

Wananchi kukamilisha Ujenzi wa Maabara



Wananchi wa Kata ya Kirua Wilayani Siha pamoja na Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Fuka wamekubaliana kwa kauli moja kukamilisha kazi ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya Sayansi katika shule hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Wananchi hao walipokuwa Wakiongea katika Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Siha alioufanya katika shule ya Sekondari Fuka tarehe 16.5.2017.

Awali Mkuu wa Shule hiyo  mwalimu Swalehe Kombo  alisoma taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa Maabara katika shule hiyo ambapo alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 5 zimetumika katika kuendeleza ujenzi wa maabara katika kipindi cha Novemba,2016 hadi Mei 15,2017.

Mkuu wa Shule hiyo alimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa,  Wananchi wa Kata ya Kirua wameweka mpango wa kupata michango ya Shilingi elfu tano kwa kila kaya ,ambapo kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kuendeleza ujenzi wa Maabara katika shule hiyo.

Akiongea na Wananchi na Wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari Fuka iliyopo   Kata ya Kirua,Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu aliwapongeza Wananchi kwa kuwa kuonyesha hali ya kujituma na moyo  ya kuchangia maendeleo hasa katika suala la elimu kwa watoto wao.

Mkuu huyo wa Wilaya alieleza kuwa Serikali itaendelea na jitihada zake za kushirikiana na Wananchi pamoja na wadau wa maendeleo katika kuleta maendeleo, na katika ujenzi wa maabara Serikali imeahidi kuleta vifaa vyote katika maabara hizo.  Alifafanua kuwa vifaa vya maabara vitakavyoletwa na Serikali ni vya gharama kubwa na vitahitaji kutunzwa na kuhifadhiwa kwa uangalifu na shule husika zitakazokabidhiwa.

Wilaya ya Siha inajumla ya shule 13 za Serikali ambapo kila shule inahitaji kuwa na maabara 3 kwa masomo ya Biolojia,Chemia na Fizikia kama ilivyo agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Friday, 12 May 2017

Serikali Wilaya ya Siha kuboresha miundombinu ya soko Sanya Juu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa  jumla ya fedha za kitanzania milioni  71  ili kuboresha miundombinu katika soko la Sanya Juu Wilayani Siha.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Onesmo Buswelu akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyasema hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Alieleza kuwa kazi hiyo inatarajiwa kuanza hivi karibuni na kutaka taratibu na kuanza kazi hiyo zifanyike kwa haraka na kwa kuzingatia taratibu zilizopo ili kuepukana makosa na hoja mbalimbali za ukaguzi.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali zinatumika vizuri ili kutoa thamani halisi ya fedha hizo.

Kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo kutasaidia kuondoa adha na changamoto mbalimbali zilizopo katika soko hilo hasa nyakati za mvua nyingi kama ilivyo sasa.

Siha yaboresha ongezeko la Dawa katika Zahanati na Vituo vya Afya vya Umma

Hospital ya Wilaya ya Siha imeongeza manunuzi na upatikanaji wa Dawa za binadamu kwa asilimia 85 hadi kufikia mwezi Mei ,2017 kutoka asilimia 25 mwaka 2016.

Ongezeko hili limetokana na usimamizi mzuri unaofanywa na viongozi wa Serikali katika Wilaya ya Siha hasa katika kuhakikisha kuwa Wananchi na Wakazi wa Siha wanaendelea kupata dawa na matibabu ya uhakika katika Hospital za Umma.

Taarifa ya kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa katika Zahanati,Vituo vya Afya na Hospital ya Serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kuhusu shughuli za maendeleo zilizotekelezwa na Serikali Wilaya ya Siha tangu Oktoba ,2015 chini ya Serikali ya awamo ya tano inayoongozwa na Mhe.Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wananchi Wilayani Siha watakiwa kuchukua tahadhari ya Mvua zinazoendelea kunyesha

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu amewataka wakazi na Wananchi wa Wilaya ya Siha kuchukua tahadhari ya kutosha wakati huu mvua zinapoendelea kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.

Hayo ameyasema wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo wa Serikali Wilayani Siha. Mhe Mkuu wa Wilaya ya Siha ameyasema hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha wakati alipohudhuria ufungaji wa mafunzo ya wataalam wa ugavi na manunuzi yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Siha.

Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuwalinda watoto wao nyakati za kwenda shule na wakati wa kurudi nyumbani ili wasipatwe na janga la kuzolewa na maji ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilayani hapa.

Wednesday, 12 April 2017

Wananchi wa Siha Wafanya kweli ujenzi wodi ya Wazazi

 Baadhi ya sehemu ya Wananchi wa Kata ya Sanya Juu Wilaya ya Siha wakishiriki katika kuchimba msingi utakaotumika katika ujenzi wa wodi ya Wazazi katika Hospital ya Wilaya ya Siha. Zaidi y Shilingi milioni 297 zitatumika katika ujenzi wa wodi ya Kinamama,Shilingi milioni 80 wodi ya watoto na milioni 511 zitatumika katika ujenzi wa jengo la upasuaji.Kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuwapunguzia wananchi wa Siha gharama za usafiri na matibabu ya kwenda hospital ya Mawenzi na KCMC mjini Moshi.

 Wananchi wa Kata ya Sanya Juu Wilayani Siha wakishiriki katika nguvu kazi za kuanza kwa ujenzi wa wodi ya Wazazi katika Hospital ya Wilaya ya Siha.tukio hili limefanyika hivi karibuni ambapo viongozi mbalimbali walishirikiana na Wananchi katika kazi za kujitolea
Wananchi wakiendele na kazi za kuandaa msingi wa ujenzi wa wodi ya Kinamama

Monday, 10 April 2017

Picha za mafunzo ya manunuzi ya Umma kwa Wakuu wa shule za sekondari na Wenyeviti wa bodi za Shule Wilaya ya Siha

 Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Onesmo Buswelu(wa kwanza kushoto) akishiriki katika mafunzo yanayohusu manunuzi ya Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha leo jumanne tarehe 10.4.2017
 Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya manunuzi ya Umma Tanzania mhe.Godfrey Mbanyi akitoa mafunzo ya masuala ya manunuzi ya Umma kwa wahasibu wa Halmashauri,wakuu wa shule za sekondari Siha na Wenyeviti wa bodi za shule za sekondari Wilaya ya siha.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha wakisikiliza mafunzo ya masuala ya manunuzi ya Umma

Tuesday, 4 April 2017

Picha za matukio ya jinsi Wananchi wa Wilaya ya Siha walivyoshiriki katika kuanza kwa ujenzi ya wodi ya Kinamama

 Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Onesmo Buswelu akishiriki ktk uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi ya wodi ya kinamama.zoezi hilo limefanyika leo humans tarehe 4.4.2017  ktk hospital ya Wilaya ya Siha na Kuhudhuriwa na Wananchi wengi wa Kata ya Sanya Juu.
 Baadhi ya kinamama wakishiriki katika kazi za uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi huo
 Mhe.Juma Jani Diwani wa Kata ya Sanya Juu akishiriki katika kazi ya ujenzi ya wodi hiyo mapema Leo jumanne tarehe 4.4.2017

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha Mhe.Frank Tarimo akishiriki vema katika kazi za uchimbaji wa msingi mapema Leo asbh katika eneo inapojengwa wodi ya Kinamama
 Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Onesmo Buswelu(aliyeshika kipaza sauti) akiwashukuru wananchi waliofika na kushiriki katika hatua za awali za kuchimba msingi wa wodi ya Kinamama iliyoanzwa kujengwa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ,Ujenzi na Mazingira Halmashauri ya Siha Mhe.Robert Mrisho akishiriki katika shughuli za kazi zilizokuwa zinendelea katika viwanja vya Hospital ya Wilaya ya Siha
 Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ,Afya na Maji Mhe.Witson Nkini akimwagilia maji mti alioupanda karibu na eneo inapojengwa wodi ya Kinamama


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha  Valerian Juwal akishiriki katika kazi za mikono za kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya Kinamama.kazi hiyo imefanyika mapema leo jumanne tarehe 4.4.2017 katika eneo la Hospital ya Wilaya lililopo Kata ya Sanya Juu Wilayani Siha