Tuesday, 9 June 2015

SIHA YAPATA TUZO USAFI WA MAZINGIRA 2015

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Gharib Bilal akimkabidhi  cheti cha ushindi wa tatu kwa vijiji bora kwa afya na Usafi wa Mazingira Tanzania bara   mratibu wa Kampeni ya Usafi na mazingira Wilayani Siha, Bi Joyce Tarimo.Kijiji cha mawasiliano kata ya gararagua kilishika nafasi ya tatu kitaifa na kwanza katika mikoa ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania

Saturday, 6 June 2015

MAANDALIZI YA ZOEZI LA UANDIKISHAJI LAENDELEA VIZURI SIHA

watendaji wa zoezi la uandikishaji kwa ajili ya uchaguzi Mkuu  Wilayani Siha wakila kiapo cha uaminifu kwa zoezi hilo mbele ya msimamizi mkuu Wilaya ya Siha Mkurugenzi Mtendaji

watendaji wa zoezi la uandikishaji wa uchaguzi mkuu Wilaya ya Siha  kwa mfumo mpya wa kiteknolojia wakipata mafunzo ya zoezi hilo

Friday, 5 June 2015

SIHA YAPATA KIJIJI BORA KWA USAFI WA MAZINGIRA


KIJIJI CHA MAWASILIANO CHASHIKA NAFASI YA 3 KWA USAFI TANZANIA

Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imezidi kutia fora katika siku ya Mazingira Duniani iliyoazimishwa jijini Tanga baada ya kijiji cha MAWASILIANO kata ya Gararagua kushika nafasi ya Tatu kwa vijiji visafi kabisa Tanzania bara na kuziacha Wilaya Kongwe hapa Nchini  zikishangaa mafanikio hayo.Kijiji cha kwanza Tanzania ni Sorera-Kondoa namba mbili ni kijiji cha Image-Njombe

Mafanikio ya Kijiji cha Mawasiliano yametokana na ushirikiano mkubwa kati ya Wananchi wa kata ya Gararagua,Viongozi wote wa Kijiji,na Vitongoji pamoja na uongozi mzima wa Wilaya ya Siha

"SIHA MBELE DAIMA"

WANANCHI WA SIHA WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU





                       
                                                                                                               TAREHE 05.6.2015

TANGAZO KWA UMMA
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA WILAYA YA SIHA WENYE UMRI WA MIAKA 18 AU ZAIDI KUWA,ZOEZI LA UANDIKISHAJI KWA AJILI YA KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU LITAANZA TAREHE 12/06/2015 HADI TAREHE 12/7/2015.

WANANCHI WOTE WENYE SIFA  MNATAKIWA KUTUMIA MUDA ULIOPANGWA WA KUJIANDIKISHA VIZURI ILI MUWEZE KUTUMIA HAKI YENU YA KIDEMOKRASIA YA KUCHAGUA VIONGOZI MNAOWATAKA KWA AJILI YA MAENDELEO YA WILAYA YA SIHA
NAWATAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA ZOEZI HILI MUHIMU

LIMETOLEWA NA
RASHID S KITAMBULIO
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
SIHA