HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA
MAWASILIANO: Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji(W) TEL: 027- 2757646
S. L. P. 129,
Fax: 027 2756863
Sanya Juu,
Mobile:073-
2973257
SIHA.
E-mail:dedsiha@yahoo.com
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb Na SDC/S.10/2/VOL
III/51 Tarehe 22/12/2014
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb Na SDC/S.10/2/VOL
III/51 Tarehe 22/12/2014
UTEKELEZAJI WA KIBALI CHA AJIRA
SIHA.
YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha anawatangazia ajira Wananchi wenye sifa za
kujaza nafasi za kazi zilizo orodheshwa hapa chini watume maombi.
1. Afisa Mtendaji Kata II Nafasi 1 (TGS II)
Sifa
zinazotakiwa
·
Mwombaji awe na Elimu ya Shahada / Stashahada
ya juu katika moja ya fani ya Utawala,
Rasilimali watu Sheria Elimu ya Jamii
Maendeleo ya Jamii , Usimamizi wa Fedha
Uchumi na Mipango kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
Majukumu
·
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao na
kuwa Mlinzi wa Amani katika Kata.
·
Katibu wa
Kamati ya Maendeleo ya Kata
·
Kuandaa Mpango Kazi wa Maendeleo ya kata na
kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa Afisa Tarafa
·
Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote kwenye Kata
·
Mratibu na msimamizi wa upangaji wa Mipango
shirikishi na shughuli nyingine za Maendeleo katika ngazi ya Kata
·
Kuandaa na kupendekeza maoni ya kutengeneza Sheria
Ndogo na kuyawasilisha katika Halmashauri za Wilaya / Miji
·
Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria
, kanuni na miongozo ya Serikali katika Kata
·
Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa
shughuli za Maendeleo katika Kata
·
Mwenyekiti wa Vikao vya Wataalamu katika ngazi ya
Kata,Vijiji/ Mitaa na Asasi zisizo za Kiserikali
·
Kupokea na kutatua matatizo/ malalamiko ya Wananchi
katika Kata.
2. Afisa Mtendaji Kijiji II Nafasi 11 (TGS C)
Sifa
zinazotakiwa
·
Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne au sita
aliyehitimu stashahada katika fani ya Utawala , Sheria , Elimu ya Jamii ,
Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha
Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu
·
Kusimamia Ulinzi na usalama wa Raia na mali zao
kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
·
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa
Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
·
Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashuri ya
Kijiji
·
Kutafsiri na kusimamia Sera , Sheria na Taratibu
·
Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika
Kijiji
·
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote
za nyaraka za Kijiji
·
Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za Kijiji
3. Katibu Mahsusi III Nafasi 4 (TGS B)
Sifa
zinazotakiwa
·
Waombaji
wawe na Elimu Kidato cha nne (Form IV)
·
Waombaji wawe wamehudhuria mafunzo ya uhazili na
kufaulu mitihani ya hatua ya tatu
·
Waombaji wawe wamefaulu somo la Hatimkato na
Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.
·
Waombaji wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka
Chuo chochote kinachotambulika na Serikali
·
Waombaji wawe wamepata cheti katika programu za
windows, Microsoft office , Internet E- Mail na Publisher
Majukumu
·
Kuchapa barua , taarifa na nyaraka za kawaida
·
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na
kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
·
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada ,
nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini
·
Kusaidi kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi
kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu
kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao
·
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa
walio sehemu alipo , na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu
zinazohusika
4. Msaidizi wa kumbukumbu II Nafasi 2 (TGS B)
Sifa zinazotakiwa
·
Waombaji wawe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV)
·
Waombaji wawe na cheti cha Utunzaji kumbukumbu
katika mojawapo ya fani za Afya, Masijala na Mahakamani na Ardhi.
Majukumu
·
Kutafuta kumbukumbu / nyaraka / mafaili
yanayohitajiwa na wasomaji
·
Kuchambua , kuorodhesha na kupanga ( classification and boxing) kwa
ajili ya matumizi ya Ofisi
·
Kuweka / kupanga kumbukumbu / nyaraka katika reki (
file racks/cabinets) katika masijala / vyumba vya kuhifadhi kumbukumbu
·
Kuweka kumbukumbu ( barua , nyaraka nk) katika
mafaili
5. Mchapa hati II Nafasi 1 (TGS B)
Sifa
zinazotakiwa:
·
Mwombaji awe amehitimu Kidato cha Nne au Sita
·
Mwombaji awe amefaulu Mtihani wa Uhazili hatua ya
II kutoka chuo cha Utumishi wa Umma
·
Mwombaji awe na ujuzi wa Kompyuta Hatua ya I na II kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali
Majukumu
·
Kuchapa Taarifa za uthamini na Hati za Fidia
·
Kuchapa Nyaraka na Hati za kumiliki Ardhi
Mwisho wa kutuma
maombi ni tarehe 21/01/2015.
Maombi yote
yatumwe kwa :
Mkurugenzi
Mtendaji,
Halmashauri ya
Wilaya ya Siha ,
S.L.P. 129,
Sanya Juu –Siha.
Limetolewa na:-
Rashid S. Kitambulio
Mkurugenzi Mtendaji (W)
SIHA.
No comments:
Post a Comment