Friday, 2 September 2016

WILAYA YA SIHA YASHIRIKI KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA SIKU YA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU WILAYANI HUMO

 mkuu wa Wilaya ya Siha Mh. Onesmo Buswelu ashiriki katika zoezi la upandaji miti katika shule ya Msingi Sinai kata ya Ormelili Wilayani Siha. zoezi hilo lilifanyika siku ya mbio za mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilayani Siha ukitokea mkoa wa Arusha.


Thursday, 1 September 2016

RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA FUPI WILAYANI SIHA NA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO PAMOJA NA KUKUTANA NA WANANCHI

 RC KILIMANJARO  MH. SAIDI MECKY SADIK AKIONGEA NA WANANCHI WA SIHA MAGHARIBI KATIKA KIJIJI CHA NGARENAIROBI HIVI KARIBUNI.







 RC KILIMANJARO AKIPOKEWA  KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA SIHA,ALIPOTEMBELEA HOSPITAL HIYO NA KUKAGUA HUDUMA MBALIMBALI ZINAZOTOLEWA KATIKA HOSPITAL HIYO YA WILAYA YA SIHA.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA ZAHANATI YA MAGADINI WILAYANI SIHA MKOA WA KILIMANJARO TAREHE 28.8.2016






JENGO LA MAKAZI YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NAMWAI LAFUNGULIWA NA MWENGE WA UHURU WILAYANI SIHA MKOA WA KILIMANJARO

 Jengo la nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Namwai Kata ya Ngarenairobi lililofunguliwa na mwenge wa Uhuru Wilayani Siha. jengo hilo lina uwezo wa kuishi walimu sita kwa wakati mmoja. mwenge wa uhuru ulifungua jengo hilo tarehe 28.8.2016 uliwasili Wilayani Siha.

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA KWA SHANGWE NA WANANCHI WA WILAYA YA SIHA MKOANI KILIMANJARO

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SIHA VALERIAN JUWAL AKIPOKEA MWENGE WA UHURU KATIKA KIJIJI CHA MATADI TAREHE 28.8.2016

MWENGE WA UHURU WAZINDUA NA KUFUNGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYANI SIHA MKOA WA KILIMNAJRAO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH. 1.4 BILIONI











Wednesday, 31 August 2016

MIRADI YA MAENDELEO YA ZAIDI YA TSH. 1.4 BILIONI YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU WILAYANI SIHA

Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Siha ulizindua,kufungua na kuweka mawe ya msingi kwa jumla ya miradi sita yenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya 1.4 bilioni.

Mwenge wa uhuru ulipokelewa Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Wilayani Siha ukitokea Mkoa wa Arusha tarehe 28.8.2016 na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi wa Tarafa ya Siha Magharibi katika kijiji cha Matadi,Kata ya Ndumet.

Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Wilaya ya Siha ulikimbizwa katika maeneo mbalimbali yaWilaya ya Siha na kufungua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya Elimu Kata ya Ngarenairibi,Maji kata ya Karansi, ,Afya kata ya Gararagua,mradi wa vijana kata ya Sanya Juu,Barabara kata ya Livishi na Madarasa manne shule ya msingi Sinai kata ya Ormelili na baadaye mwenge ulikesha katika kituo cha Mabasi Orkolili KIA.

katika maeneo yote mwenge ulipopita Wilayani Siha Wananchi walijitokeza kwa wingi katika mapokezi ya kuulaki mwenge wa uhuru kama ishara ya kudumisha umoja,mshikamano na amani ya Taifa la Tanzania


kufungua ,kuzindua