Wednesday, 31 August 2016

MIRADI YA MAENDELEO YA ZAIDI YA TSH. 1.4 BILIONI YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU WILAYANI SIHA

Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Siha ulizindua,kufungua na kuweka mawe ya msingi kwa jumla ya miradi sita yenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya 1.4 bilioni.

Mwenge wa uhuru ulipokelewa Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Wilayani Siha ukitokea Mkoa wa Arusha tarehe 28.8.2016 na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi wa Tarafa ya Siha Magharibi katika kijiji cha Matadi,Kata ya Ndumet.

Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Wilaya ya Siha ulikimbizwa katika maeneo mbalimbali yaWilaya ya Siha na kufungua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya Elimu Kata ya Ngarenairibi,Maji kata ya Karansi, ,Afya kata ya Gararagua,mradi wa vijana kata ya Sanya Juu,Barabara kata ya Livishi na Madarasa manne shule ya msingi Sinai kata ya Ormelili na baadaye mwenge ulikesha katika kituo cha Mabasi Orkolili KIA.

katika maeneo yote mwenge ulipopita Wilayani Siha Wananchi walijitokeza kwa wingi katika mapokezi ya kuulaki mwenge wa uhuru kama ishara ya kudumisha umoja,mshikamano na amani ya Taifa la Tanzania


kufungua ,kuzindua

No comments:

Post a Comment