Saturday, 6 June 2015

MAANDALIZI YA ZOEZI LA UANDIKISHAJI LAENDELEA VIZURI SIHA

watendaji wa zoezi la uandikishaji kwa ajili ya uchaguzi Mkuu  Wilayani Siha wakila kiapo cha uaminifu kwa zoezi hilo mbele ya msimamizi mkuu Wilaya ya Siha Mkurugenzi Mtendaji

watendaji wa zoezi la uandikishaji wa uchaguzi mkuu Wilaya ya Siha  kwa mfumo mpya wa kiteknolojia wakipata mafunzo ya zoezi hilo

Friday, 5 June 2015

SIHA YAPATA KIJIJI BORA KWA USAFI WA MAZINGIRA


KIJIJI CHA MAWASILIANO CHASHIKA NAFASI YA 3 KWA USAFI TANZANIA

Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imezidi kutia fora katika siku ya Mazingira Duniani iliyoazimishwa jijini Tanga baada ya kijiji cha MAWASILIANO kata ya Gararagua kushika nafasi ya Tatu kwa vijiji visafi kabisa Tanzania bara na kuziacha Wilaya Kongwe hapa Nchini  zikishangaa mafanikio hayo.Kijiji cha kwanza Tanzania ni Sorera-Kondoa namba mbili ni kijiji cha Image-Njombe

Mafanikio ya Kijiji cha Mawasiliano yametokana na ushirikiano mkubwa kati ya Wananchi wa kata ya Gararagua,Viongozi wote wa Kijiji,na Vitongoji pamoja na uongozi mzima wa Wilaya ya Siha

"SIHA MBELE DAIMA"

WANANCHI WA SIHA WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU





                       
                                                                                                               TAREHE 05.6.2015

TANGAZO KWA UMMA
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA WILAYA YA SIHA WENYE UMRI WA MIAKA 18 AU ZAIDI KUWA,ZOEZI LA UANDIKISHAJI KWA AJILI YA KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU LITAANZA TAREHE 12/06/2015 HADI TAREHE 12/7/2015.

WANANCHI WOTE WENYE SIFA  MNATAKIWA KUTUMIA MUDA ULIOPANGWA WA KUJIANDIKISHA VIZURI ILI MUWEZE KUTUMIA HAKI YENU YA KIDEMOKRASIA YA KUCHAGUA VIONGOZI MNAOWATAKA KWA AJILI YA MAENDELEO YA WILAYA YA SIHA
NAWATAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA ZOEZI HILI MUHIMU

LIMETOLEWA NA
RASHID S KITAMBULIO
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
SIHA

Sunday, 17 May 2015

ZITAMBUE KATA ZILIZOPO WILAYA YA SIHA




KATA ZA WILAYA YA SIHA         

1.     BIRIRI 
2.     DONYOMURAK 
3.     GARARAGUA 
4.     IVAENY 5.     KARANSI 
6.     KASHASHI 
7.     KIRUWA 
8.     LIVISHI 
9.     MAKIWARU 
10.  MITIMIREFU 
11.  NASAI 
12.  NDUMET 
13.  NGARENAIROBI 
14.  OLKOLILI 
15.   SANYA JUU





 NB: Pamoja na Kata 15 Wilaya ya Siha pia ina jumla ya vijiji 60, Vitongoji 169 na Jimbo moja la Uchaguzi, Idadi ya watu kutokana na Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012  ni 116,313 wanaume 56500 na Wanawake ni 59813

USAILI AJIRA MADEREVA WILAYA YA SIHA



HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

                                                                                                                          12.05.2015

TANGAZO LA USAILI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha anawatangazia  usaili wa kazi ya udereva  utakaofanyika  Tarehe 15.05.2015.  Wafuatao wanatakiwa  kufika  Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha muda wa saa mbili (2:00) asubuhi.

1.       ABDALLAH JUMA MKAMBI
2.       ABDI SHABANI  MWANSANGA
3.       BAHATI BENESI KAMAGA
4.       BIUCLANDE DANIEL PALLANJO
5.       CHARLES RICHARD MTERA
6.       DANNY DANIEL
7.       ELIAS ELISA KIMARO
8.       EVARIST ALOYCE ASSEY
9.       GEORGE P LUEAS
10.   HENRY MARTIN SOLOMON
11.   JAPHET BRYSON MSUYA
12.   JOHN E MAHUNDI
13.   JOHN LECK TEMU
14.   JOSHUA PETER LUKONDE
15.   KEPHA ARTHUR  JUSTO
16.    RAJABU HAMIS
17.   WILBERT FREDRICK MAIM
18.   YOENI A MBWAMBO

NB:Tafadhali fika na vyeti Halisi vya kusomea (original certificates) pamoja na Leseni ya udereva

NB:Tangazo hili pia linapatikana kwenye blog  ya Halmashauri ya Siha, ingia google, andika :sihaleo.blogspot.com

Limetolewa na


Rashid S Kitambulio
                                                        Mkurugenzi Mtendaji (W) Siha