Magadini Sekondari waongoza matokeo ya ”mock” kidato cha 6 mkoa wa Kilimanjaro 2018
Hatimaye shule ya Kata ya Magadini Sekondari Wilaya ya Siha
imefanikiwa kuongoza katika matokeo ya utamirifu (Mock) katika mkoa wa
Kilimanjaro kati ya shule 66 za kidato cha sita zilizofanya mtihani.
Kwa mujibu wa matokeo ya mock mkoa wa Kilimanjaro
yaliyotolewa hivi karibuni,shule hiyo ya Kata imefanikiwa kuzipiku shule kongwe
hapa Nchini zikiwemo shule ya Ufundi Moshi,Umbwe,Ashira,Weruweru na nyingine
nyingi.
Akizungumzia matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Siha Valerian Juwal aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kazi nzuri
waliyofanya ya kuiletea sifa Wilaya ya Siha na Kata ya Gararagua kwa ujumla
wake.
No comments:
Post a Comment