SIHA YAPATA MAFANIKIO ZOEZI LA KUPIGA
CHAPA MIFUGO
Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa
Kilimanjaro imefanikiwa katika zoezi la kupiga chapa ng’ombe wenye umri wa
miezi 6 au zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Siha Valerian Juwal akitoa taarifa ya zoezi hilo akiwa katika ofisi za
Halmashauri ya Siha.
Alieleza kuwa hadi kufikia tarehe 30/1/2018
ng’ombe 25735 sawa na asilimia 84 walikuwa wametambuliwa kwa kupigwa chapa
pamoja na kuvalishwa hereni.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akishiriki zoezi la kupiga chapa mifugo kijiji cha Lekrimuni Wilaya ya Siha mwishoni mwa mwaka 2017 |
Zoezi la kutambua na kupiga chapa ng’ombe
Wilaya ya Siha lilianza rasmi tarehe 1/11/2017 ambapo lengo lilikuwa ni kupiga
chapa ng’ombe 30,538 wenye umri wa zaidi ya miezi sita.
Ratiba ya kupiga chapa iliwekwa na wataalam wa mifugo kwa kushirikiana na
watendaji wa Vijiji na Kata kwa Vijiji vyote 60,kata 17 na vitongoji 169
vilivyopo katika Wilaya ya Siha.
No comments:
Post a Comment