Saturday, 28 June 2014

 mwenyekiti wa kamati ya wa Elimu afya na Maji wilaya ya Siha Witson Nkini akitoa zawadi kwa Baadhi ya shule  za msingi zilifanya vizuri katika mashindano ya usafi Wilaya ya Siha


wanachama wa chama cha kuweka na kukopa kwa Walimu wa Siha na Hai wakiwa katika kikao chao cha mwaka katika ukumbi wa RC sanya juu hivi karibuni


wanachama hao wakicheza mziki kufurahia matunda ya chama chao ambacho kwa sasa kina zaidi ya wanachama 1700



ofisa wa elimu wilaya ya Siha Kushoto aliyevaa blauzi ya rangi ya maziwa Rozi Sandi akishiriki zoezi la kutoa zawadi kwa washindi wa mazingira katika shule za Msingi hivi karibuni

Saturday, 7 June 2014

HABARI KATIKA PICHA

Mkuu wa Polisi wilaya ya Siha Afande Mwakyusa akikagua mzoga wa Tembo aliyekutwa amekufa mazingira ya kutatanisha kijiji cha karansi hivi karibuni.Wengine ni wananchi wa kijiji hicho walishuhudia tukio hilo




wanafunzi wa shule ya Sekondari Sanya Juu(Sanya Day) wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa siku
ya mazingira duniani iliyofanyika tarehe 05.06.2014 kwa zoezi la kupanda miti katika shule hiyo.zoezi hili liliwezeshwa na Jumuiya ya benki ya wananchi tanzania COBAT 


 

mwakilishi wa COBAT Bi Hellen Anchasein akipanda miti kati shule ya Sekondari Suumu katika maazimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe 05,06.2014


wanafunzi wa shule ya sekondari sanya Juu wakishiriki katika zoezi la uhifadhi wa mazingira katika kilele cha siku ya mazingira Duniani tarehe 05.06.2014
 zoezi la mazingira sanya Juu Sekondari





kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya siha Eliot Mwasbwite aliyevaa miwani kushoto alionesha masikitiko yake baada ya kufika eneo la tukio alipokufa tembo katika mazingira yasiyoeleweka

Saturday, 17 May 2014

baadhi ya watumishi wa Wilaya ya siha waliofika katika moja ya vilele vya mlima kilimanjaro siku ya ijumaa tarehe 16.05.2014 katika kuitikia wito wa kuboresha utalii wa ndani ulitolewa na TANAPA


vijana wa wilaya ya Siha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo ya utunzaji wa fedha yaliyotolewa na COBAT kwa ushirikaino na We Effect kutoka Sweden..mwenye nywele nyeupe wa Nne kutoka kulia ni Fuhanael Kihunrwa mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo haya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Amani sanya Juu

Monday, 12 May 2014







jengo la kisasa la hospital mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha linalotegemewa kutumika katika siku za hivi karibuni katika kuimarisha huduma za afya kwa Wananchi wa Siha



wananchi wa kijiji cha Wiri kata ya Gararagua wakiitikia wito wa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro wa Kuotesha miti katika maeneo mbalimbali ya kuzunguka eneo la ofisi ya kijiji cha Wiri





HILI NI LANNGO LA LONDOROSI GETI SEHEMU AMBAYO ITATUMIKA KUPANDA MLIMA  KILIMANJARO KATI YA TAREHE 15-18 2014 NA WATALII WA NDANI KUTOKA MKOA WA KILIMNAJARO (PICHA HAPA CHINI)






HALI ILVYOKUWA KATIKA UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI 2014


Saturday, 3 May 2014

ZOEZI LA UPANDAJI MITI KATIKA KATA YA GARARAGUA,KIJIJI CHA WIRI WILAYA YA SIHA

Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa akipokea taarifa fupi ya upandaji wa Miti katika Kata ya Gararagua iliyopo Wilayani Siha.zoezi hili limefanyika mwishoni mwa wiki
mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Wilaya ya siha ndugu Jonas  P.M akieleza jambo katika zoezi la upandaji miti kijiji cha Wiri mbele ya mkuu wa Wilaya ya Siha ambaye pichani hayupo

SHEREHE ZA MEI MOSI 2014 UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI

WAFANYAKAZI WAKIPONGEZANA KATIKA SHEREHE ZILIFANYIKA UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI.
BANGO LA WAFANYAKAZI KUTOKA HOSPITAL YA KIBONGOTO WILAYANI SIHA WAKIPITA MBELE YA MGENI RASMI NA UJUMBE WA MEI MOSI2014
SHAMBA LA MISITU WILAYANI SIHA LILILOPO WEST KILIMANJARO WAKIPITA MBELE YA MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA WAKIWA NA GARI LENYE MICHE YA MITI KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI MWAKA 2014


bango la hospital ya taifa ya Kifua Kikuu iliyopo Wilayani Siha Wakitoa ujumbe wao kwa Wafanyakazi katika maadhimisho ya Mei Mosi 2014 katika Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi

HABARI KATIKA PICHA


























mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha Mheshimiwa Jonathan Nasari alisoma Taarifa yake mbele ya Baraza la Madiwani Siha tarehe 30.04.2014
BAADHI YA MADIWANI WA VITI MAALUMU WAKITETA JAMBO MARA BAADA YA KIKAO CHA  BARAZA LA MADIWANI TAREHE 30 04. 2014 KATIKA HALMASHAURI YA SIHA