KERO ZA WALIMU
KUSHUGHULIWA SIHA
Kero mbalimbali za walimu katika Halmashauri
ya Wilaya ya siha kuendelea kushughulikiwa kwa karibu zaidi ili kuongeza
kiwango cha ufaulu kwa shule za msingi na Sekondari.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal
mapema leo tarehe 4 desemba 2017 katika ukumbi wa mikutano wa RC Sanya Juu
alipokutana na walimu wa shule za msingi kwa lengo la kufanya tathmini ya
matokeo ya darasa la saba mwaka 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha
aliwataka walimu Wilaya ya Siha kufanya kazi kwa bidii na maarifa huku
wakizingatia maadili ya kazi ya ualimu kwani taifa na jamii linawategemea
walimu.
Alitoa wito kwa walimu wote wenye kero
mbalimbali zinazowasumbua kufika ofisi ya mkurugenzi wakati wowote kwani ofisi
yake ipo tayari kupokea na kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali za walimu Wilaya
Siha.
Hata hivyo,alieleza kuwa yapo matatizo na
kero za walimu ambazo ofisi yake imekwisha zitatua mara baada ya kuzipokea kero
hizo, naomba kutoa wito kwa walimu kutumia hata namba yangu ya simu kunipigia
pale wanapoona kuwa hawapati huduma stahiki katika ofisi wanazofanyia kazi
alisema Juwal.
Katika Tathmini hiyo ya matokeo ya darasa la
saba kwa shule za msingi Siha mwaka 2017 shule zilizofanya vizuri ni pamoja na PUNCMI,SAMAKI,NGARONY,NKYARE,GARARAGUA,KYENGIA,FUKA
ENG MED, LOKIRI NA FUKA.
No comments:
Post a Comment