Jumla ya Wanafunzi 2304
wanatarajiwa kumaliza elimu ya msingi katika shule mbalimbali za msingi
Halmashauri ya Wilaya ya Siha kwa mwaka 2017. Kati ya wanafunzi hao wavulana ni
1137 na wasichana ni 1167.
Wanafunzi hao wanatarajiwa
kufanya mitihani hiyo ya taifa ya
kuhitimu masomo ya shule za msingi kwa
muda wa siku mbili tarehe 6/09/2017 na
tarehe 07/09/2017.
Mitihani hiyo ya taifa itafanyika
katika vituo 55 vilivyopangwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha, kati ya
vituo hivyo 52 ni shule za Serikali ambao watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili
na vituo 3 binafsi na Taasisi za Kidini ambazo ni English Medium .
No comments:
Post a Comment