Halmashauri ya Wilaya ya
Siha kueneza tekinolojia mpya ya kilimo na ufugaji bora katika ngazi ya Halmashauri ,
Kata na hatimaye katika vijiji vyote.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Valerian Juwal alipokuwa
katika kilele cha maonesho ya nanenane yaliyofanyika kikanda katika viwanja vya
Njiro Arusha ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Siha ilipata fursa ya kuonesha
tekinolojia mbalimbali ya kilimo na mifugo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Siha alisema kuwa Halmashauri ya Siha itahakikisha kuwa mashamba
Darasa yaliyopo kila kata yanaendelezwa ili kuwanufaisha wananchi wa maeneo
husika na vijiji jirani.
Alieleza kuwa Halmashauri
ya Wilaya ya Siha itawatumia wataalam wa kilimo na mifugo waliopo katika ngazi
ya Halmashauri ,Kata na Vijiji kuhakikisha wakulima wanapatiwa utaalam na
ushauri wa kilimo na ufugaji wa kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya
kilimo na ufugaji.
Juwal aliwataka wananchi
kuondokana na kilimo na ufugaji wa
kitamaduni na badala yake wabadilike na kuanza kulima na kufuga kwa kufuata
tekinolojia mpya ambazo zitawasaidia kuongeza kipato na kuondokana na kuwa na
vipato duni.
Mkurugenzi wa halmashauri
ya Siha ametoa wito kwa viongozi mbalimbali Wilayani Siha kuendelea
kuwahamasisha wananchi kuzingatia ushauri wanaopewa na wataalam wa kilimo na
mifugo waliopo katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa
mazao ya kilimo na mifugo pia.
Zaidi ya asilimia 90 ya
wananchi wa Wilaya ya Siha wanategemea kilimo na ufugaji kama shughuli kubwa za
kiuchumi kwa wananchi hao.mazao yanayolimwa kwa wingi zaidi ni
Mahindi,maharage,viazi,ndizi,ngano,shairi na mazao ya mbogamboga.
No comments:
Post a Comment