Wednesday, 11 May 2016

KIDATO CHA SITA WAMALIZA MITIHANI YAO SHULE 4 ZA SIHA

Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule za Sekondari wilayani Siha wahitimu mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2016 katika shule Nne za Sekondari Wilayani hapa.

Ofisa Elimu Sekondari Abrahaman Kanji alizitaja shule hizo kuwa ni Shule ya Sekondari Sanya Juu(Sanya Day),Oshara,Visitation na Faraja Siha.

alieleza kuwa kwa ujumla mitihani imefanyika kwa kufuata utaratibu unaotakiwa na baraza la mitihani la Taifa kwa kuzingatia maelekezo ,taratibu na Sheria zote za Mitihani ya Taifa kufanyika.

Kati ya Shule hizo nne Mbili zinamilikiwa na  Serikali na nyingine na mashirika ya Dini. Wilaya ya Siha inajumla ya shule 6 za kidato cha tano na Sita  4 za Serikali na 2 za mashirika ya Dini zenye kuchukua wanafunzi katika michepuo ya masomo ya  Sayansi na Sanaa.

1 comment: