Wednesday 5 October 2016

SIHA YACHANGIA ZAIDI YA TSH.17.5 MIL MAAFA YA KAGERA

zaidi ya Tsh. 17.5 milioni zimepatikana kama mchango wa Wananchi,Wadau wa Maendeleo na Watumishi katika Halmashauri ya  Wilaya ya Siha kwa ajili ya kuchangia waathirika wa maafa ya Tetemeko lililotokea Mkoa wa Kagera hivi karibuni.

Fedha hizo zimepatika kupitia michango ya hiari kutoka kwa wadau wa maendeleo pamoja na wakazi na wananchi wa Wilaya ya Siha ambao kwa umoja wao wamekuswa na tukio hilo na kuamua kutoa mchango wa fedha kwa ajili ya kusaidia Wananchi wa Mkoa wa kagera walioguswa na janga hilo.

kwa mujibu wa mwenyekiti wa Maafa katika Wilaya ya Siha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Onesmo Buswelu ,Fedha hizo zimeshatumwa kwa wahusika kupitia akaunti husika kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Siha imepata pongezi nyingi kutoka ofisi yaMkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa jinsi wananchi wake na wadau mbalimbali wa maendeleo walivyoguswa na kutoa michango yao kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na Wilaya nyingine hapa Mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment