Tuesday 11 October 2016

MPANGO WA PAMOJA TUWALEE ULIOTEKELEZWA WILAYANI SIHA TANGU 2010

PAMOJA TUWALEE: Ulikuwa mpango wa kitaifa wa miaka 6 wa huduma na matunzo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na ulianza Wilayani Siha mwaka 2010

lengo la mpango huu likiwa ni kuboresha maisha kimwili,kijamii,na kiuchumi kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na familia zao

mpango huu pia umetengenezwa kwa kufuata na kuzingatia miongozo ya Serikali ya Tanzania na mfadhili ambaye ni Rais wa Marekani ukiwa na lengo la kusaidia majanga yatokanayo na ukimwi.

Katika Wilaya ya Siha umeweza kufika katika Kata zote 12 ambayo ni sawa  na asilimia 71 ya kata zote 17 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Siha.

pia mpango huu umeweza kufika na kufanya kazi katika vijiji 39 sawa na asilimia 65 kati ya vijiji vyote 60 Halmashauri ya Wilaya ya Siha


No comments:

Post a Comment