Monday, 31 October 2016
MPANGO WA PAMOJA TUWALEE WILAYANI SIHA
Mwenyekiti wa HALMASHAURI ya SIHA Mhe. Frank Tarimo(wa tatu kutoka kushoto) akifurahia Jambo katika shughuli za Kupokea taarifa ZA mpango wa pamoja Tuwalee zilizomaliza muda wake kwa miaka mitano katika HALMASHAURI ya Wilaya ya SIHA. Mpango huu ulikuwa NA jukumu la kuwawezesha watoto WANAOISHI katika mazingira hatarishi Wilayani SIHA NA limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Wananchi wapata elimu ya kujikinga NA ugonjwa wa TB (kifua kikuu)
Wataalam wa AFYA katika hospital ya Taifa ya kifua kikuu kibongoto Wilayani SIHA WAKITOA elimu kwa umma kwa njia ya igizo ya namna bora ya kujikinga NA ugonjwa wa TB ambao unaambukiza kwa njia ya Hewa. Igizo hilo lilifanyika mbele ya mgeni rasmi mhe. Hamis Kigwangalla Naibu waziri wa AFYA,maendeleo ya JAMII,jinsia,Wazee NA watoto alipokuwa hospitalini hapo hivi karibuni ktk zoezi la kuzindua bodi ya hospital hiyo longer hapa Nchini.
Vitalu bora vya MICHE ya miti Shamba la miti West Kilimanjaro
Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya SIHA wakiangalia jinsi wataalam wa utunzaji wa MICHE ya miti katika Shamba la miti West KILIMANJARO wanavyofanya kazi hiyo
WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI SIHA WAKITOA UJUMBE KWA JAMII KWA NJIA YA NYIMBO
wanafunzi wa shule ya sekondari Sanya Juu wakitoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya nyimbo katika moja ya makongamano yaliyofanyika Wilayani Siha hivi karibuni.
vitalu vya miche ya miti shamba la miti West KILIMANJA
BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU YAZINDULIWA RASMI
SIHA YAPOKEA MADAWATI 200 KUTOKA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA KWA AJILI YA SHULE 5 ZA MSINGI
![]() |
MKUU WA WILAYA YA SIHA MHE ONESMO BUSWELU (KULIA) AKIPOKEA MADAWATI 200 KUTOKA MENEJA WA SHAMBA LA MITI WEST KILIMANJARO KWA NIABA YA WAKALA WA MISITU TANZANIA |
BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONGOTO YAZINDULIWA RASMI
MHE. HAMIS KIGWANGALLA NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AZINDUA BODI YA HOSPITAL YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONGOTO.TUKIO HILO LIMEFANYIKA MWISHONI MWA WIKI
![]() |
MHE HAMIS KIGWANGALLA (KULIA) NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AKIFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA SIHA |
![]() |
MHE. HAMIS KIGWANGALLA NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO AKIPOKELEWA KATIKA WILAYA YA SIHA |
MHE HAMIS KIGWANGALLA (kulia) AKITOA MAELEKEZO YA KAZI ALIPOFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU KATIKA HOSPITAL MPYA YA WILAYA YA SIHA MWISHONI MWA WIKI
WADAU WACHANGIA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI WILAYANI SIHA-PICHA
![]() |
DIWANI WA KATA YA GARARAGUA MHE. ZACHARIA LUKUMAY AKITOA NENO WAKATI WA HARAMBEE YA KUKUSANYA FEDHA ZA KUKARABATI MIUNDOMBINU CHAKAVU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI |
![]() |
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SIHA VALERIAN JUWAL AKITOA MAELEKEZO YA SERIKALI ALIPOKUWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI WILAYANI SIHA |
![]() |
WAJUMBE WA BODI NA VINGOZI WENGINE WA SERIKALI WALIPOKUWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MAGADINI HIVI KARIBUNI |
Thursday, 27 October 2016
HABARI KATIKA PICHA
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA VALERIAN JUWAL AKITOA NENO KATIKA KILELE CHA KUFUNGA MPANGO WA PAMOJA TUWALEE ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA SIHA HIVI KARIBUNI
VIONGOZI MBALIMBALI WA WILAYA NA HALMASHAURI YA SIHA SIKU YA KUFUNGA MPANGO WA PAMOJA TUWALEE ULIODUMU WILAYA YA SIHA KWA MUDA WA MIAKA MITANO. MPANGO HUU ULIKUWA UNASAIDIA KUWAWEZESHA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI CHINI YA UFADHILI WA WATU WA MAREKANI
MATUKIO KATIKA PICHA
sehemu ya bustani ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha -Kilimanjaro katika maonesho ya kilimo nanenane Arusha kwa mwaka huu 2016(picha Maktaba )
muonekano wa banda la Halmashauri ya Wilaya ya Siha -Kilimanjaro katika maonesho ya kilimo nanenane Arusha kwa mwaka 2016 (picha maktaba)
Hawa ni baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro wakiwa katika mazoezi ya kawaida kwa ajili ya kuboresha afya zao(picha maktaba yetu)
mchezo wa magunia ni miongoni mwa michezo isiyopewa kipau mbele hapa nchini na Duniani lkn kwa upande wa watumishi wa Halmashauri ya Siha wameamua kuundeleza mchezo huu. picha ya bonanza la michezo mwishoni mwa mwaka jana(picha maktaba yetu)
watumishi wa halmashauri ya Siha wakiwa katika maandalizi ya kufanya mazoezi ya kukimbia kwa gunia kwa upande wa wanaume(picha ya maktaba)
muonekano wa banda la Halmashauri ya Wilaya ya Siha -Kilimanjaro katika maonesho ya kilimo nanenane Arusha kwa mwaka 2016 (picha maktaba)
Hawa ni baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro wakiwa katika mazoezi ya kawaida kwa ajili ya kuboresha afya zao(picha maktaba yetu)
mchezo wa magunia ni miongoni mwa michezo isiyopewa kipau mbele hapa nchini na Duniani lkn kwa upande wa watumishi wa Halmashauri ya Siha wameamua kuundeleza mchezo huu. picha ya bonanza la michezo mwishoni mwa mwaka jana(picha maktaba yetu)
watumishi wa halmashauri ya Siha wakiwa katika maandalizi ya kufanya mazoezi ya kukimbia kwa gunia kwa upande wa wanaume(picha ya maktaba)
Monday, 24 October 2016
WADAU WACHANGIA ELIMU WILAYANI SIHA-KILIMANJARO
Wadau wachangia elimu
shule ya sekondari Magadini
Wadau mbalimbali wa elimu Wilayani Siha wamechangia fedha za
ukarabati wa miundombinu ya shule ya Sekondari Magadini iliyopo Kata ya
Gararagua Wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro.
Harambee hiyo iliandaliwa na Bodi ya Shule ya Sekondari
Magadini kwa ushirikiano na Uongozi wa Shule hiyo pamoja na uongozi wa Kata na Vijiji.
Katika harambee hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
Shule ya Sekondari Magadini zaidi ya Tsh. Milioni 5 zilikusanywa, fedha
hizi zinajumuisha fedha taslimu,ahadi na
vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wadau .
Awali akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi katika harambee hiyo mkuu
wa shule Felista Kileo alieleza kuwa
wameona ni vema kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuunga mkono
jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha miundombinu ya shule
hiyo ili kuboresha mazingira ya
kujifunza na kufundishia.
Alieleza kuwa fedha na vifaa mbalimbali vilivyopatikana
vitasaidia katika kuboresha na kukarabati madarasa kachakavu katika shule hiyo
yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.
Katika harambee hiyo ,Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo
Buswelu alichangia mifuko 35 ya saruji yenye thamani ya shilingi 525,000/=
ambapo mchango wake ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Siha.
Monday, 17 October 2016
UFUGAJI WA NYUKI WASAIDIA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KIJIJI CHA MATADI- WEST KILIMANJARO
BAADHI YA WAFUGAJI NYUKI KIJIJI CHA MATADI WAKITUNDIKA MIZINGA YA NYUKI KATIKA MAENEO YALIYOTUNZWA MAZINGIRA VIZURI
WANANCHI WA KIJIJI CHA MATADI WAKIFURAHIA UTUNZAJI MZURI WA MAZINGIRA ULIVYOSAIDIA ONGEZEKO LA UPATIKANAJI WA ZAO LA ASALI KATIKA KIJIJI CHAO
WAFUGAJI WA NYUKI WAKIPATA ASALI MARA BAADA YA ZOEZI LA URINAJI WA ASALI KUFANYIKA. |
WAFUGAJI WA NYUKI KIJIJI CHA MANIO WAPATIWA MIZINGA YA KISASA ZAIDI YA 40
DIWANI WA KATA YA KASHASHI MHE. SUZAN NATAI AKIPOKEA MIZINGA YA KISASA ZAIDI YA AROBAINI KWA AJILI YA WANANCHI WAKE WA KIJIJI CHA MANIO |
DIWANI WA KATA YA KASHASHI SUZAN NATAI AKISHUKURU HALMASHAURI YA SIHA KWA KUWAPATIA WAFUGAJI WA NYUKI KTK KIJIJI CHAKE MIZINGA YA KISASA |
MWAKILISHI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA SIHA DR BARNABAS MBWAMBO AKITUNDIKA MIZINGA KATIKA KIJIJI CHA MANIO KATA YA KASHASHI |
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA UFUGAJI NYUKI ERNEST MARANDU AKITOA MAELEZO YA MATUMIZI YA MIZINGA ILIYOKABIDHIWA NA HALMASHAURI YA SIHA KWA WAFUGAJI WA KIJIJI CHA MANIO KATA YA KASHASHI |
MIZINGA ILIYOTUNDIKWA NA WAFUGAJI WA NYUKI KIJIJI CHA MANIO MARA BAADA YA KUKABIDHIWA |
UTUNZAJI WA MAZINGIRA KIJIJI CHA MANIO- WILAYANI SIHA WASAIDIA WAFUGAJI WA NYUKI
baadhi ya wafugaji wa Kijiji cha Manio wakisubiri kukabidhiwa mizinga katika kijiji chao |
UTENZI WA KUMUENZI BABA WA TAIFA MWL JULIUS K NYERERE
UTENZI
WA KUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA MWL
JULIUS K NYERERE 14/10/2016
1. Naanza kwa kumsifu,
Mungu wetu Mtukufu,
Yeye ni fundi Sanifu,
Sisi tumeumbwa naye.
2. Namtaja wetu Mungu,
Aliyekuwe tangu ,
Amezitundika Mbingu,
Ardhi katugawia.
3. Kwake yeye tunaishi,
Sisi kwake watumishi,
Wala hakuna ubishi,
Pumzi katujalia.
4. Mungu huyu ana utu,
Anazo nafsi tatu,
Roho,mwana,baba yetu,
Mola mmoja sikia.
5. Huyu ni wetu mkubwa,
Anayetoa ubwabwa,
Siriye imesiribwa,
Hakuna wa kufasiri.
6. Ba’da ya kumshukuru,
Mungu bila ya kukufuru,
Sasa ninayanukuru,
Niliyoyakusudia.
7. Nianze kusimulia,
Tendo la kihistoria,
Kifupi nitayasogoa,
Sikilizeni kwa makini.
8. Kwanza twarejea nyuma,
Kwa makini kutozama,
Tulivyofanywa wanyama,
Katika yetu aridhi.
9. Mkoloni kang’ang’ania,
Nchi akaikalia,
Wakaumia raia,
Wasijue la kufanya.
10. Akatokea kijana,
Mwenye upeo mpana,
Kasema tutapambana,
Tanganyika tuwe huru.
11. Namtaja Juliasi,
Huyu ndiye muasisi,
Kasema siyo rahisi,
Lakini tutaupata.
12. Mkoloni kakasirika,
Akaitwa kibaraka,
Mroho wa madaraka,
Tena asiyetosheka.
13. Wakoloni wauaji,
Ni wakubwa wanyonyaji,
Baba kawavua taji,
Uhuru tukaupata.
14. Tarehe tisa disemba,
Wananchi tukaimba,
Tukacheza na sindimba,
Uhuru kushangilia.
15. Falsafa ya ujamaa,
Ndiyo ilikuwa taa,
Pia kujitegemea,
Iwe ndio yetu njia.
16. Lugha yetu Kiswahili,
Ni mkubwa mhimili,
Juliasi kakubali,
Iunganishe raia.
17. Ni mwana diplomasia,
Mpenda Demokrasia,
Haki zote za raia,
Yeye aliyepigania.
18. Usawa wa Binadamu,
Kaka dada na binadamu,
Sote tushike hatamu,
Kuleta maendeleo
19. Na elimu ya Msingi,
Aliyesema mambo mengi,
Isiwekewe vigingi,
Ni haki ya kila
mtu.
20. Nchi zote kapitia,
Afrika nzimasikia,
Hamasa akiwatia,
Lazima wajitawale.
21. Kasema Afrika viva,
Kongo mambo yakaiva,
Msumbiji,Angola viva,
Zimbabwe na Namibia.
22. Pote aliheshimika,
Wakawa na uhakika,
Bendera wakasimama,
Hongera baba Nyerere.
23. Jama huu ni utenzi,
Una nyingi sana beti,
Ninalikunja busati,
Wengine wamalizie,
24. Mengi nimeelezea,
Kuwachosha siyo nia,
Kwa hapa nitakomea,
Hadi wakati mwingine.
Imeandaliwa na kusomwa na:
MWL
JUSTINA MOHAMED NGOLINDA
SHULE
YA Sekondari Oshara-SIHA KILIMANJARO
PICHA ZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA WILAYANI SIHA
![]() |
Mmoja wa watoa mada Katika maadhimisho ya baba wa Taifa Wilayani Siha (Mwl Ngolinda wa Shule ya Sekondari Oshara) akitoa mada namna anavyomfahamu baba wa Taifa |
![]() |
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Sanya Juu wakitumbuiza katika maadhimisho ya kumkumbuka ya Baba wa Taifa Wilaya ya Siha. |
![]() |
Wanafunzi wa Halaiki Wilayani Siha wakitoa ujumbe wa mshikamano na upendo kama ishara ya kumkumbuka baba wa Taifa Mwl Julius K Nyerere. |
![]() |
mmoja wa washiriki (Mzee Daniel Sandewa) kwa niaba ya wazee wa Siha akitoa neno la Shukurani kwa Wananchi wa Siha kwa namna walivyoshiriki vema katika kumkumbuka baba wa Taifa la Tanzania |
Subscribe to:
Posts (Atom)