Friday, 12 July 2019
Pata matokeo ya Kidato cha Sita shule za Sekondari Siha mwaka 2019
Bofya hapa kuona Matokeo ya shule za Siha
http://www.sihadc.go.tz/new/angalia-matokeo-kidato-cha-sita-2019-shule-za-siha
matukio ya Mwenge wa Uhhuru wapokelewa kwa Shangwe Wilayani Siha
Wananchi wa Kata ya Ndumeti walivyoupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilaya ya Siha mwaka 2019
Wananchi wa Kijiji cha Matadi Kata ya Ndumeti walivyopokea Mwenge wa Uhuru katika shule ya Sekondari matadi ulipowasili shuleni hapo tarehe 20.6.2019
Kata ya Ndumeti kijiji cha Matadi ilivyotia fora katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2019
Madiwani Siha wapanga mkakati wa kuimarisha mapato ya ndani ya Halmashauri
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Siha wakisikiliza Mawasilisho ya miradi mkakati inayotarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Siha -Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu akiongea na Waheshimiwa Madiwani walipokuwa katika mkutano wa kawaida wa baraza tarehe 11.7.2019
Waheshimu Madiwani wa Halmashauri ya Siha wakiwa katika mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani Siha tarehe 11.7.2019
Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe.Onesmo Buswelu akisema jambo katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Siha tarehe 11.7.2019
ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Siha tarehe.7.7.2019
Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe Onesmo Buswelu akimpokea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Siha tarehe 7.7.2019
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha mhe. Godson Ngomuo akimpokea katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa
Katibu Tawala wa Wilaya ya Siha Joseph Mabiti akisalimiana na katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa ndugu Bashiru Ally akisalimiana na Wakuu wa Idara na Vitengo alipowasili katika Hospitali ya Wilaya ya Siha
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Siha Dkt. Barnabas Mbwambo akisalimiana na Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa
Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Godwin Mollel (katikati ) akipokea burudani kutoka ngoma za kabila la Kimaasai walipompokea katibu mkuu wa CCM Taifa
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bashiru Ally akifurahia ngoma ya kimaasai alipowasili katika Hospital ya Wilaya ya Siha
Monday, 13 May 2019
WATUMISHI WANAMICHEZO SIHA WAFANYA ZIARA HIFADHI YA NGORONGORO
Timu ya mpira wa miguu ya watumishi wa Umma ikijiandaa na mchezo wa Bonanza
tarehe 4/5/2019 kati ya timu himu na Serena Hotel Timu
Wachezaji wa Siha wakipeana mbinu za mchezo wakati wa mapumziko
Kikosi kamili cha watumishi wa Siha kilichosafiri kwenda kwenye Bonanza la michezo hifadhi ya Ngorongoro kuanzia tarehe 3/5/2019 hadi tarehe 5/5/2019
Mazoezi kabla ya mchezo ndiyo njia bora ya kuweka miili katika hali bora zaidi,timu ya Siha hapo juu ikijifua kabla ya mchezo wa Bonanza
Thursday, 25 April 2019
BARABARA ZA SIHA ZABORESHWA
Wakala wa usimamizi wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Siha wameendelea kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano kwa vitendo kwa kuzifanyia matengenezo barabara za vijijini katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Siha.
Kwa Ujumla barabara zote katika Vijiji na Vitongoji Wilayani Siha zinapitika wakati wote na kusaidia shughuli mbalimbali za wananchi katika kusafiri na kusafirisha mazao mbalimbali ya biashara na chakula
Hii ni barabara ya Siha Sango hadi Kijiji cha Mese Wilayani Siha ikiendelea kufanyiwa matengenezo makubwa kupitia TARURA
WAZAZI WATAKIWA KUWAPA ELIMU WATOTO BILA UBAGUZI-SIHA
Wananchi wa Wilaya ya Siha wameshauriwa kuwapa watoto wote elimu bila ubaguzi wa aina yoyote
Hayo yamesemwa na Mwalimu Rose Sandi Afisa elimu shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilayani ya Siha leo tarehe 2.04.2019 aliposhiriki na watoto wenye mahitaji maalumu (siku ya Usonji) katika maazimisho ya siku yao duniani.
Watoto wenye usonji wakishirikiana na wazazi wao katika zoezi la kupanda miti mapema leo katika shule ya msingi Sanya Juu
Maazimisho hayo katika Wilaya ya Siha yamefanyika katika shule ya Msingi Sanya juu na kujumuisha watoto wenye mahitaji maalumu kutoka shule mbalimbali za msingi Wilayani Siha ikiwemo shule ya Msingi Faraja Siha .
Wanafunzi wa shule ya msingi Sanya Juu wakishiriki maazimisho ya siku ya Usonji dunia leo tarehe 2.4.2019
Katika Maazimisho hayo wazazi na jamii imetakiwa kuwapa elimu watoto wote katika familia bila ubaguzi wa jinsia,maumbile au uwezo wa watoto katika kuelewa na kuchanganua mambo mbalimbali.
Subscribe to:
Posts (Atom)


































