Tuesday, 9 October 2018

SIHA YAPOKEA MIL 500 UJENZI HOSPITAL YA WILAYA


Siha yapokea Mil 500 ujenzi Hospital ya Wilaya

Serikali ya Tanzania inayoongozwa na  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika hospital ya Wilaya ya Siha.

Mkurugenzi Mtendajji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Ndg, Valerian Juwal aliyasema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Siha kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Siha tarehe 08/10/2018.

Aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa, kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha miundombinu ya majengo katika hospital  ya Wilaya ya Siha, ambapo zaidi wa wakazi 120,000 wa Wilaya ya Siha  wanapata huduma za afya katika Hospital ya Wilaya.

“Napenda kumshukuru Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoendelea kuwaletea wananchi wa Wilaya ya Siha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya  maendeleo ikiwemo miradi ya Maji,Elimu,Afya,miundombinu ya barabara” alisema Juwal.


Wednesday, 31 January 2018

Picha za ujenzi wa barabara ya Lami Sanya Juu Elerai

Mitambo mikubwa ikiwa katika ujenzi  barabara kwa kiwango cha Lami eneo la Datch Kona karibu na makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha.barabara hii inajengwa na Fedha za Serikali ya Tanzania kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 52

Mashine aina ya Greda ikiwa katika eneo la Mwisho wa lami Wilaya ya Siha ikiendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.jumla ya kilomita 32.3 zinatarajiwa kujengwa kuanzia mwisho wa Lami hadi Elerai

Miundombinu bora yachangia kiwango cha ufaulu shule za Siha

Mojawapo ya maabara bora kabisa iliyopo katika shule ya sekondari Nuru  Wilaya ya Siha. kuwepo kwa maabara kama hii kumechangia kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutoa vifaa vya maabara katika maabara zote zilizokamilika hapa nchini. shule ya sekondari Nuru Wilaya ya Siha ni mojawapo ya shule zilizonufaika na mpango wa Serikali wa kupatiwa vifaa vya maabara.

zoezi la kupiga chapa Siha lafikia asilimia 84



SIHA YAPATA MAFANIKIO ZOEZI LA KUPIGA CHAPA MIFUGO

Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imefanikiwa katika zoezi la kupiga chapa ng’ombe wenye umri wa miezi 6 au zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Valerian Juwal akitoa taarifa ya zoezi hilo akiwa katika ofisi za Halmashauri ya Siha.

Alieleza kuwa hadi kufikia tarehe 30/1/2018 ng’ombe 25735 sawa na asilimia 84 walikuwa wametambuliwa kwa kupigwa chapa pamoja na kuvalishwa hereni.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akishiriki zoezi la kupiga chapa mifugo kijiji cha Lekrimuni Wilaya ya Siha mwishoni mwa mwaka 2017


Zoezi la kutambua na kupiga chapa ng’ombe Wilaya ya Siha lilianza rasmi tarehe 1/11/2017 ambapo lengo lilikuwa ni kupiga chapa ng’ombe 30,538 wenye umri wa zaidi ya miezi sita.

Ratiba ya kupiga chapa iliwekwa  na wataalam wa mifugo kwa kushirikiana na watendaji wa Vijiji na Kata kwa Vijiji vyote 60,kata 17 na vitongoji 169 vilivyopo katika Wilaya ya Siha.

Wilaya ya Siha yapanda katika ufaulu bora kidato cha Nne 2017

 wanafunzi wa shule za sekondari Wilaya ya Siha



SIHA YASHIKA NAFASI 2 MKOA NA 16 KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2017
Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa mapema jana na baraza la mtihani ya taifa Tanzania(NECTA),Halmashauri ya Wilaya ya Siha imendelea kutamba kwa kushika nafasi za juu katika matokeo hayo.

Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya baraza la mitihani la Tanzania,Wilaya ya Siha imeshika nafasi ya 16 Nchini Tanzania kati ya Halmashauri,Majiji na Manispaa 195 zilizopo.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Mkoa wa kilimanjaro umeshika nafasi ya kwanza kitaifa ukifuatiwa na Mkoa wa Pwani, huku mkoa ukijinasua kutoka nafasi ya 5 mwaka 2016 hadi nafasi ya kwanza mwaka 2017.

Pamoja na matokeo hayo Wilaya ya Siha imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwa nafasi ya kwanza imeshikwa Moshi Vijijini.

Siha yafanya kweli matokeo kidato cha Nne 2017



Siha yashika nafasi pili Mkoa wa Kilimanjaro  matokeo kidato cha Nne 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imeshika nafasi ya pili kati ya Halmashauri 7 za mkoa wa Kilimanjaro matokeo kidato cha nne.

Kwa mujibu ya matokeo yaliyotolewa na tovuti ya baraza la mitihani la taifa mapema jana,Halmashauri ya Siha imepanda kutoka nafasi ya 40 kitaifa mwaka 2016  hadi nafasi ya 16 mwaka 2017.

Halmashauri ya Siha inazo jumla ya shule 18 za Sekondari kati ya hizo 13 za Serikali na shule  4 za mashirika ya dini  na shule  moja inamilikiwa na mtu binafsi.


Monday, 15 January 2018

Nafasi ya shule za Siha Kidato cha Sita

Nafasi shule za Siha matokeo Mock kidato cha Sita 2018
1.MAGADINI Sekondari  nafasi (1) Kiwilaya na nafisi ya (1) Kimkoa
2.OSHARA Sekondari nafasi ya (2) Kiwilaya na nafasi ya (8) Kimkoa
3.MAGNIFICAT Sekondari nafasi ya (3) Kiwilaya na nafasi ya (38) Kimkoa
4.SANYA JUU  Sekondari nafasi ya (4) Kiwilaya na nafasi ya (53) Kimkoa
5. VISITATION GIRLS Sekondari nafasi ya (5) Kiwilaya na nafasi ya (55) Kimkoa
6.FARAJA SIHA Sekondari nafasi ya (6) Kiwilaya na nafasi ya (59) Kimkoa
7.NURU Sekondari nafasi ya (7) Kiwilaya na nafasi ya (65) Kimkoa