Thursday, 23 September 2021

Dkt. Mollel mbunge wa Jimbo la Siha ahimiza mshikamano zaidi kwa Wananchi

 Mbunge wa Jimbo la Siha mkoa wa Kilimanjaro mhe. Dkt.Godwin Mollel amewataka wananchi na wakazi wa jimbo la Siha kuendeleza mshikamano zaidi kwa lengo la kupata maendeleo 

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni alipokuwa katika kikao cha Wah. Madiwani wa Halmashauri ya Siha kilichofanyika makao makuu ya Halmashauri ya Siha.

Wilaya ya  Siha ni miongoni mwa Wilaya iliyopiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro licha ya kuwa miongoni mwa Wilaya  mpya katika Mkoa wa Kilimanjaro 

No comments:

Post a Comment