Wednesday 31 January 2018

zoezi la kupiga chapa Siha lafikia asilimia 84



SIHA YAPATA MAFANIKIO ZOEZI LA KUPIGA CHAPA MIFUGO

Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imefanikiwa katika zoezi la kupiga chapa ng’ombe wenye umri wa miezi 6 au zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Valerian Juwal akitoa taarifa ya zoezi hilo akiwa katika ofisi za Halmashauri ya Siha.

Alieleza kuwa hadi kufikia tarehe 30/1/2018 ng’ombe 25735 sawa na asilimia 84 walikuwa wametambuliwa kwa kupigwa chapa pamoja na kuvalishwa hereni.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akishiriki zoezi la kupiga chapa mifugo kijiji cha Lekrimuni Wilaya ya Siha mwishoni mwa mwaka 2017


Zoezi la kutambua na kupiga chapa ng’ombe Wilaya ya Siha lilianza rasmi tarehe 1/11/2017 ambapo lengo lilikuwa ni kupiga chapa ng’ombe 30,538 wenye umri wa zaidi ya miezi sita.

Ratiba ya kupiga chapa iliwekwa  na wataalam wa mifugo kwa kushirikiana na watendaji wa Vijiji na Kata kwa Vijiji vyote 60,kata 17 na vitongoji 169 vilivyopo katika Wilaya ya Siha.

No comments:

Post a Comment