Wednesday 31 January 2018

Wilaya ya Siha yapanda katika ufaulu bora kidato cha Nne 2017

 wanafunzi wa shule za sekondari Wilaya ya Siha



SIHA YASHIKA NAFASI 2 MKOA NA 16 KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2017
Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa mapema jana na baraza la mtihani ya taifa Tanzania(NECTA),Halmashauri ya Wilaya ya Siha imendelea kutamba kwa kushika nafasi za juu katika matokeo hayo.

Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya baraza la mitihani la Tanzania,Wilaya ya Siha imeshika nafasi ya 16 Nchini Tanzania kati ya Halmashauri,Majiji na Manispaa 195 zilizopo.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Mkoa wa kilimanjaro umeshika nafasi ya kwanza kitaifa ukifuatiwa na Mkoa wa Pwani, huku mkoa ukijinasua kutoka nafasi ya 5 mwaka 2016 hadi nafasi ya kwanza mwaka 2017.

Pamoja na matokeo hayo Wilaya ya Siha imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwa nafasi ya kwanza imeshikwa Moshi Vijijini.

No comments:

Post a Comment