Wednesday, 31 January 2018
Miundombinu bora yachangia kiwango cha ufaulu shule za Siha
![]() |
Mojawapo ya maabara bora kabisa iliyopo katika shule ya sekondari Nuru Wilaya ya Siha. kuwepo kwa maabara kama hii kumechangia kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi |
zoezi la kupiga chapa Siha lafikia asilimia 84
SIHA YAPATA MAFANIKIO ZOEZI LA KUPIGA
CHAPA MIFUGO
Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa
Kilimanjaro imefanikiwa katika zoezi la kupiga chapa ng’ombe wenye umri wa
miezi 6 au zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Siha Valerian Juwal akitoa taarifa ya zoezi hilo akiwa katika ofisi za
Halmashauri ya Siha.
Alieleza kuwa hadi kufikia tarehe 30/1/2018
ng’ombe 25735 sawa na asilimia 84 walikuwa wametambuliwa kwa kupigwa chapa
pamoja na kuvalishwa hereni.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akishiriki zoezi la kupiga chapa mifugo kijiji cha Lekrimuni Wilaya ya Siha mwishoni mwa mwaka 2017 |
Zoezi la kutambua na kupiga chapa ng’ombe
Wilaya ya Siha lilianza rasmi tarehe 1/11/2017 ambapo lengo lilikuwa ni kupiga
chapa ng’ombe 30,538 wenye umri wa zaidi ya miezi sita.
Ratiba ya kupiga chapa iliwekwa na wataalam wa mifugo kwa kushirikiana na
watendaji wa Vijiji na Kata kwa Vijiji vyote 60,kata 17 na vitongoji 169
vilivyopo katika Wilaya ya Siha.
Wilaya ya Siha yapanda katika ufaulu bora kidato cha Nne 2017
![]() |
wanafunzi wa shule za sekondari Wilaya ya Siha |
SIHA YASHIKA NAFASI 2
MKOA NA 16 KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2017
Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa mapema
jana na baraza la mtihani ya taifa Tanzania(NECTA),Halmashauri ya Wilaya ya
Siha imendelea kutamba kwa kushika nafasi za juu katika matokeo hayo.
Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya baraza la mitihani la
Tanzania,Wilaya ya Siha imeshika nafasi ya 16 Nchini Tanzania kati ya
Halmashauri,Majiji na Manispaa 195 zilizopo.
Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Mkoa wa kilimanjaro umeshika
nafasi ya kwanza kitaifa ukifuatiwa na Mkoa wa Pwani, huku mkoa ukijinasua
kutoka nafasi ya 5 mwaka 2016 hadi nafasi ya kwanza mwaka 2017.
Pamoja na matokeo hayo Wilaya ya Siha imefanikiwa kushika
nafasi ya pili katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwa nafasi ya kwanza imeshikwa
Moshi Vijijini.
Siha yafanya kweli matokeo kidato cha Nne 2017
Siha yashika nafasi pili Mkoa wa Kilimanjaro matokeo kidato cha Nne 2017
Halmashauri
ya Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imeshika nafasi ya pili kati ya
Halmashauri 7 za mkoa wa Kilimanjaro matokeo kidato cha nne.
Kwa mujibu
ya matokeo yaliyotolewa na tovuti ya baraza la mitihani la taifa mapema
jana,Halmashauri ya Siha imepanda kutoka nafasi ya 40 kitaifa mwaka 2016 hadi nafasi ya 16 mwaka 2017.
Halmashauri ya
Siha inazo jumla ya shule 18 za Sekondari kati ya hizo 13 za Serikali na shule 4 za
mashirika ya dini na shule moja inamilikiwa na
mtu binafsi.
Monday, 15 January 2018
Nafasi ya shule za Siha Kidato cha Sita
Nafasi shule za Siha matokeo Mock kidato cha Sita 2018
1.MAGADINI Sekondari nafasi (1) Kiwilaya na nafisi ya (1) Kimkoa
2.OSHARA Sekondari nafasi ya (2) Kiwilaya na nafasi ya (8) Kimkoa
3.MAGNIFICAT Sekondari nafasi ya (3) Kiwilaya na nafasi ya (38) Kimkoa
4.SANYA JUU Sekondari nafasi ya (4) Kiwilaya na nafasi ya (53) Kimkoa
5. VISITATION GIRLS Sekondari nafasi ya (5) Kiwilaya na nafasi ya (55) Kimkoa
6.FARAJA SIHA Sekondari nafasi ya (6) Kiwilaya na nafasi ya (59) Kimkoa
7.NURU Sekondari nafasi ya (7) Kiwilaya na nafasi ya (65) Kimkoa
1.MAGADINI Sekondari nafasi (1) Kiwilaya na nafisi ya (1) Kimkoa
2.OSHARA Sekondari nafasi ya (2) Kiwilaya na nafasi ya (8) Kimkoa
3.MAGNIFICAT Sekondari nafasi ya (3) Kiwilaya na nafasi ya (38) Kimkoa
4.SANYA JUU Sekondari nafasi ya (4) Kiwilaya na nafasi ya (53) Kimkoa
5. VISITATION GIRLS Sekondari nafasi ya (5) Kiwilaya na nafasi ya (55) Kimkoa
6.FARAJA SIHA Sekondari nafasi ya (6) Kiwilaya na nafasi ya (59) Kimkoa
7.NURU Sekondari nafasi ya (7) Kiwilaya na nafasi ya (65) Kimkoa
Magadini Sekondari waongoza matokeo ya Utamirifu Mkoa wa Kilimanjaro 2018
Magadini Sekondari waongoza matokeo ya ”mock” kidato cha 6 mkoa wa Kilimanjaro 2018
Hatimaye shule ya Kata ya Magadini Sekondari Wilaya ya Siha
imefanikiwa kuongoza katika matokeo ya utamirifu (Mock) katika mkoa wa
Kilimanjaro kati ya shule 66 za kidato cha sita zilizofanya mtihani.
Kwa mujibu wa matokeo ya mock mkoa wa Kilimanjaro
yaliyotolewa hivi karibuni,shule hiyo ya Kata imefanikiwa kuzipiku shule kongwe
hapa Nchini zikiwemo shule ya Ufundi Moshi,Umbwe,Ashira,Weruweru na nyingine
nyingi.
Akizungumzia matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Siha Valerian Juwal aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kazi nzuri
waliyofanya ya kuiletea sifa Wilaya ya Siha na Kata ya Gararagua kwa ujumla
wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)