Tuesday 9 October 2018

SIHA YAPOKEA MIL 500 UJENZI HOSPITAL YA WILAYA


Siha yapokea Mil 500 ujenzi Hospital ya Wilaya

Serikali ya Tanzania inayoongozwa na  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika hospital ya Wilaya ya Siha.

Mkurugenzi Mtendajji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Ndg, Valerian Juwal aliyasema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Siha kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Siha tarehe 08/10/2018.

Aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa, kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha miundombinu ya majengo katika hospital  ya Wilaya ya Siha, ambapo zaidi wa wakazi 120,000 wa Wilaya ya Siha  wanapata huduma za afya katika Hospital ya Wilaya.

“Napenda kumshukuru Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoendelea kuwaletea wananchi wa Wilaya ya Siha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya  maendeleo ikiwemo miradi ya Maji,Elimu,Afya,miundombinu ya barabara” alisema Juwal.


No comments:

Post a Comment