Tuesday 9 October 2018

VIJIJI VYOTE WILAYANI SIHA VYAPATIWA UMEME


ASILIMIA 100 VIJIJI WILAYANI   SIHA VINA UMEME
Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imefanikiwa kuvipatia vijiji vyake vyote 60 nishati ya umeme (ambayo ni sawa na asilimia 100) na hivyo kuongeza kasi ya wananchi kujiendeleza kiuchumi katika sekta mbalimbali.
Hayo yametolewa   na ndg Ismael Salum Meneja wa Shirika la Umeme Wilaya ya Siha tarehe 08/09/2018 katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Siha, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Kikao hicho chini ya Mwenyekiti Mhe. Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha walitoa pongezi nyingi kwa uongozi wa shirika hilo Wilaya ya Siha kwa huduma bora wanazoendelea kuzitoa kwa wananchi.

Meneja wa shirika la umeme Wilaya ya Siha alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa maeneo yote katika Wilaya ya Siha yanakuwa na huduma ya umeme ili kuwezesha mpango wa Serikali ya Viwanda.

Wilaya ya Siha imefanikiwa kusambaza umeme kwa vijiji 60 kati ya 60 vilivyopo na hadi mwezi septemba, 2018 vitongoji 126 kati ya 169 vimepatiwa  huduma ya umeme.



No comments:

Post a Comment