Tuesday, 31 October 2017
Sunday, 29 October 2017
Kata 3 bora, Kata 3 duni matokeo Darasa la Saba 2017- Siha
Kata 3 bora matokeo Darasa la Saba 2017 -Siha
- MITIMIREFU
- LEVISHI
- KIRUA
Kata 3 duni matokeo Darasa la Saba 2017 -Siha
- DONYOMURWAK
- BIRIRI
- NDUMET
Thursday, 26 October 2017
Shule 10 bora na shule 10 duni matokeo darasa la Saba 2017 Wilaya ya Siha
Shule 10 Bora matokeo darasa la Saba 2017 -SIHA
- PUNCHMI
- SAMAKI
- NGARONY
- NKYARE
- GARARAGUA
- NURU
- KYENGIA
- FUKA ENG MED
- LOKIRI
- FUKA
- KIRISHA
- SABUKU
- KANDASHI
- DONYOMURWA
- ROSELINE
- SANYA JUU
- MAKIWARU
- KISHISHA
- NAIBILI
- EMBUKOI
Wanawake Wapatiwa Mikopo
Vikundi
22 Wanawake vyapatiwa mikopo 2016/2017
Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoa wa
Kilimanjaro imefanikiwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi 22 vya
wanawake Wilayani Siha katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha
Valerian Juwal alieleza hayo katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika
hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.
Taarifa ya Mkurugenzi mtendaji ilieleza
kuwa,katika mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri ya Wilaya ya Siha imetoa
mikopo kwa vikundi 22 vya wanawake Wilayani
Siha yenye thamani ya shilingi 56 ,000,000/=
zikiwa ni fedha kutoka mchango wa Halmashauri wa asilimia tano (5%) ya mapato yake
ya ndani.
Aidha, Mkurugenzi katika taarifa yake
alieleza Baraza kuwa pamoja na changamoto ya halmashauri kukabiliwa na vyanzo
vichache vya ukusanyaji wa mapato lakini Halmashauri imejitahidi kutoa kiasi
hicho cha fedha kwa vikundi vilivyoomba mikopo na vilivyotimiza vigezo vya
kupata mikopo hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu mbalimbali.
Ametoa wito kwa vikundi vya wanawake katika
wilaya ya Siha kutumia fursa hiyo ya Serikali ya kuomba mikopo yenye masharti nafuu katika kujikwamua kiuchumi katika ngazi ya
Familia na jamii kwa ujumla wake.
Hata hivyo,Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Siha ametoa wito kwa vikundi mbalimbali vilivyopatiwa mikopo kutumia mikopo
hiyo kwa shughuli waliojipangia badala
ya kutumia mikopo waliyopewa katika
mambo yasiyoleta tija.
Alieleza kuwa pamoja na jitihada za
halmashauri kutoa mikopo hiyo kwa wanawake lakini wahusika bado wanayo wajibu mkubwa wa
kuhakikisha kuwa mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati ili iweze kuwasaidia
wanufaika wengine katika halmashauri ya Wilaya ya Siha.
Halmashauri ya Wilaya ya Siha katika
upangaji wa mipango na bajeti kila mwaka inatenga asilimia 5 ya mapato ya ndani
kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha wanawake na asilimia 5 ya mapato ya ndani ya
Halmashauri mikopo kwa vikundi vya
vijana.
Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri
ilitenga bajeti ya Tsh 87,051,850 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake.
Ambapo hadi kufikia Juni 2017 jumla ya vikundi ishirini na mbili (22) vya
wanawake vilipatiwa mkopo wenye thamani ya Tshs 56,000,000/= zikiwa ni fedha
kutoka mchango wa Halmashauri wa asilimia tano (5%) ya mapato ya ndani.
Wednesday, 25 October 2017
Siha yafanikiwa zoezi la utoaji wa chanjo mwaka 2016/2017
Utoaji wa Chanjo Wafanikiwa
Wilaya ya Siha mwaka 2016/2017
Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imefikia
zaidi ya asimia 96 ya huduma ya utoaji
wa chanjo mbalimbali ya kujikinga na magonjwa kwa watoto Wilayani hapa.
Katika taarifa ya mwaka 2016/2017 iliyotolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Siha Valerian Juwal katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani
lililokutana mwezi Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.
Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji ilieleza kuwa katika huduma ya
utoaji wa chanjo mbalimbali kwa watoto, halmashauri ya Wilaya ya Siha
imefanikiwa kutoa chanjo ya matone ya vitamin A na dawa za minyoo hadi kufikia
asilimia 96.7
Aidha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji ilieleza kuwa,katika
huduma ya utoaji wa chanjo ya kansa ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike
wenye umri chini ya miaka 14,zoezi hilo
pia lilifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 87.
Mkurugenzi Mtendaji alieleza Baraza la Madiwani kuwa, Halmashauri ya Wilaya
ya Siha ni miongoni mwa Halmashauri za
Wilaya hapa nchini zilizofanya vizuri katika usimamiaji wa zoezi zima la utoaji
chanjo kwa watoto.
Alieleza kuwa siri ya mafanikio ya zoezi hilo ni ushirikiana wa dhati baina ya Wananchi ,viongozi na wadau wengine
wa maendeleo katika Wilaya ya Siha.
Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Siha
aliwaomba wananchi na viongozi wa Siha kuendelea kuunga mkono jitihada za
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuboresha afya ya wananchi wake
hasa utoaji wa chanjo unaosaidia kutoa kinga mbalimbali kwa watoto.
Vile vile,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha alieleza
Baraza la Madiwani kuwa huduma ya chanjo zote alizozitaja hutolewa bure kwa
kugharamiwa na Serikali na hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa mara moja
iwapo watatokea watu wanaowadai fedha za kulipia huduma hiyo.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012
Halmashauri ya Wilaya ya Siha inajumla ya watu 116,313 wakiwemo wanaume 56,500
na wanawake 59,813.
Monday, 23 October 2017
Picha matukio zoezi la usaili ajira mpya halmashauri ya Siha Oktoba 23,2017
walioitwa katika usaili Halmashauri ya Siha wakifanya usaili wa maandishi katika moja ya vyumba vilivyoandaliwa na Halmashauri ya Siha
mafuriko ya walioitwa katika usaili wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Siha mara baada ya kutoka katika usaili
Hawa ni baadhi tu ya walioitwa katika usaili katika halmashauri ya Siha wakiwa katika shule ya Sekondari Kilingi
Afisa utumishi na Utawala Nico Kayange katikati akitoa maelekezo mbalimbali kwa waliomba ajira mpya Siha
Usaili ukifanyika chini ya uangalizi makini wa Maofisa wa Halmashauri ya Siha waliokabidhiwa jukumu hilo .zoezi hilo zimeanza leo kwa mchujo wa kwanza na litaendelea hadi tarehe 25.10.2017
Sunday, 22 October 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)