Friday 8 April 2016

SIHA KUPANDA MITI ZAIDI YA 1.7 MIL






HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA
TAARIFA KWA UMMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha anapenda kuwajulisha Wananchi wote wa Wilaya ya Siha kuwa maadhimisho ya kampeni ya kupanda miti Kimkoa yatafanyika  katika Wilaya ya Siha tarehe 21/04/2016.

Katika maadhimisho hayo,Wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi katika eneo la makao makuu ya Halmashauri na katika maeneo mengine watakayoelekezwa na viongozi wao kwa ajili ya kushirikiana zoezi la kupanda miti. Mgeni rasmi  katika maadhimisho hayo atakuwa Mheshimiwa Said Meck Sadiki   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Aidha mh.mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atashiriki zoezi la kupanda miti na Wananchi eneo la makao makuu ya Halmashauri siku hiyo.

Wananchi wa maeneo Kata za jirani na Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha lililopo Kata ya Gararagua kwa jina  maarufu Dutch Kona wanaombwa kufika kwa wingi kwa ajili ya Kuunga mkono jitihada za Serikali za kutunza Mazingira
Katika maadhimisho hayo  zaidi ya miti 7,000 ya aina mbalimbali zitapandwa katika eneo la kuzunguka makao makuu ya Halmashauri ya Siha.

Aidha, Maandalizi ya kupanda miti siku hiyo yamekamilika ambapo Mkuu wa Wilaya ya Siha,Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Siha ni miongoni mwa viongozi watakaoshiriki na Wananchi katika upandaji miti.

Katika kuitikia wito wa zoezi hilo leo wanavikundi mbalimbali wa mazingira kutoka Wilaya ya Siha wamepanda miti zaidi ya 4,000 katika eneo atakalopanda miti Mh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atakapojumuika na Wananchi tarehe 21.4.2016
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ya Wilaya ya Siha imeweka malengo ya kupanda miti zaidi ya 1.7 Mil katika maeneo mbalimbali katika halmashauri hiyo
Limetolewa na
 Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya (W) Siha
Tarehe 08/4/2016

No comments:

Post a Comment