Sunday 17 April 2016

HALMASHAURI ZOTE KILIMANJARO ZATAKIWA KUWA NA BUSTANI ZA MICHE YA MITI



Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki ameagiza halmashauri zote Mkoa wa Kilimanjaro kuwa na bustani za vitalu vya miti na kugawa miti hiyo bure kwa wananchi
Hayo ameyasema alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa ambayo yalifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha tarehe 15.4.2016
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alishiriki kwa kupanda miti zaidi ya 10,000 iliyopandwa katika eneo la makao makuu ya Halmashauri ya siha, ambapo wananchi,watumishi na kikundi cha Floresta
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sasa wakati umefika kwa kila halmashauri kutenga bajeti za kuendesha bustani za vitalu vya miche ya miti itakayogawiwa bure kwa wananchi na taasisi zote za serikali hasa shule za msingi na sekondari
‘’Kanzia sasa lazima kila wilaya kuhakikisha kuwa inamiliki kitalu cha miche ya miti ambayo itasaidia upatikanaji wa miti ya kupanda hasa wakati wa msimu wa mvua kama ilivyo hivi sasa’’alisema mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Hadi sasa Halmashauri ya Wilaya ya siha inabustani ya miche ya miti ambayo inauwezo wa kuwa na miche zaidi ya 1.5Mil kwa wakati mmoja
Aidha halmashauri ya Wilaya ya Siha ilianzisha mpango wa kuwa na kitalu cha miche ya miti kinachomilikiwa na Halmashauri kuanzia mwaka 2012 na miche inayozalishwa katika kitalu hicho hugawanywa  bure kwa wananchi,Taasisi za Umma na ofisi za kata na vijiji  

No comments:

Post a Comment