Friday 18 September 2020

 

Tambua mafanikio ya Halmshauri ya Siha Sekta ya Maji yafikia asilimia 90

Katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 halmashauri ya Wilaya ya Siha imeendelea kuwa kinara katika usambazaji wa maji katika vijiji vyote 60,vitongoji 169 na Kata zote 17.

Hadi kufikia mwezi Septemba 2020 usambazaji wa maji Wilaya ya Siha umefikia  zaidi ya asilimia 90 ambapo  maji safi na salama yanapatikana wakati wote

Serikali ya awamu ya tano imetoa zaidi ya shilingi 3.7 bilioni  kwa ajili ya kugharamia  usambazaji na upanuzi wa miradi ya maji mikubwa na midogo Wilayani Siha.

Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya Uongozi dhabiti wa Serikali ya awamu ya tano ,halmashauri imejipanga kuhakikisha usambazaji wa maji unaongezeka hadi zaidi ya asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.

No comments:

Post a Comment