Wednesday, 23 December 2020
Wednesday, 7 October 2020
Friday, 2 October 2020
Halmashauri ya Siha yapongezwa na kuboresha stendi ya mabasi Sanya Juuu
Wakazi na Wananchi wa Wilaya ya Siha wameendelea kutoa pongezi kwa Halmashauri ya Siha kwa kuboresha kituo cha Mabasi Sanya Juu. Wanachi hao hasa madereva na wamiliki wa magari ya abiria katika nyakati tofauti wameeleza kufurahishwa na miundombinu bora na imara iliyopo katika stendi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli akiwa na viongozi wa dini hivi karibuni ambapo walitembelea stendi hiyo alieleza kuwa Halmashauri ya Siha imetumia zaidi ya shilingi Milioni 4 ya mapato ya ndani katika kuboresha miundombinu ya Stendi ya Sanya Juu na ile ya KIA.
WANAFUNZI 2357 KUHITIMU ELIMU YA MSINGI SIHA 2020
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli amesema kuwa kati ya wanafunzi 2357 watakaomaliza darasa la saba tarehe 7-8/10/2020 wasichana ni 1230 na wavulana ni 1127 katika shule za msingi 59,Shule za Serikali 53 na za mashirika na dini na binafsi ni shule 06
Maandalizi ya kufanyika kwa mtihani huo yameshakamilika na matarajio ya Halmashauri ni kuendelea kupata matokeo mazuri na kushika nafasi za juu kimkoa na Kitaifa alisema ndugu Ndaki Mhuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha
Friday, 18 September 2020
UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI-SIHA
Katika kipindi cha miaka 5 ya Serikali ya awamu ya tano Halmashauri ya Siha imefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 154 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu vyenye wanufaika 2,629 ambapo jumla ya kiasi cha shilingi 439,399,843 zilitolewa na Halmashauri kutoka mapato ya ndani.
Fedha zilizotolewa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Siha kwa kuzingatia utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020
Tambua
mafanikio ya Halmshauri ya Siha Sekta ya
Maji yafikia asilimia 90
Katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 halmashauri ya Wilaya
ya Siha imeendelea kuwa kinara katika usambazaji wa maji katika vijiji vyote
60,vitongoji 169 na Kata zote 17.
Hadi kufikia mwezi Septemba 2020 usambazaji wa maji Wilaya ya
Siha umefikia zaidi ya asilimia 90
ambapo maji safi na salama yanapatikana
wakati wote
Serikali ya awamu ya tano imetoa zaidi ya shilingi 3.7
bilioni kwa
ajili ya kugharamia usambazaji na
upanuzi wa miradi ya maji mikubwa na midogo Wilayani Siha.
Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya Uongozi
dhabiti wa Serikali ya awamu ya tano ,halmashauri imejipanga kuhakikisha
usambazaji wa maji unaongezeka hadi zaidi ya asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.
Mafanikio
ya Halmshauri ya Siha Sekta Barabara 2015-2020
Katika kipindi cha
miaka mitano Halmasauri ya Siha imepokea kiasi cha shilingi 57.2 bilioni kutoka
Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati a miundombinu ya barabara kwa kiwango
cha lami,changarawe na ukarabati wa
barabara vijijini.
Fedha zilizotolewa na
Serikali ya Tanzania zimesaidia ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa km
32.2 kutoka Sanya Juu hadi Elerai,ujenzi wa barabara za changarawe vijijini jumla
ya km 199.2.
Pia Serikali ya awamu
ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. John
Magufuli imewezesha Madaraja muhimu kama
vile Kisube kirisha, Lawate loiwang, Muri - Nkwamariko na
Mwaru.
Aidha,Serikali
ya Tanzania kupitia wakala wa Barabara TARURA imefanikiwa kufanya ukarabati wa barabara
zenye urefu wa km 236.81 na kuifanya
halmashauri ya Siha kuwa miongoni mwa Halmashauri hapa nchini zenye barabara
zinazopitika wakati wote wa mwaka.
Mafanikio
haya yote yametokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Wananchi wa
Wilaya ya Siha pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya
Wilaya.