Wednesday, 15 March 2017
Watendaji wa Kata na Vijiji Halmashauri ya Siha watakiwa kutenda kazi kwa uadilifu
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha akifungua mafunzo kwa watendaji wa Vijiji na Kata zote Halmashauri ya Siha
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Valerian Juwal amewataka watendaji wa vijiji na Kata kufanya kazi za Umma kwa kuzingatia kanuni,taratibu,miongozo na Sheria za utumishi wa Umma.
Akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha , Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal aliwataka watendaji wa vijiji na Kata kuzingatia yale yote yatakayofundishwa kuanzia mwanzo wa mafunzo hadi mwisho wa mafunzo.
Aliwataka watendaji hao kuwa mfano mwema wa kutenda Hali hasa suala la kusimamia ulinzi wa amani pamoja na kusimamia vema ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri katika maeneo yao ya kazi
Aidha ,aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia agizo la Serikali ya awamo ya tano kuhusu upigwaji marufuku wa matumizi ya madawati ya kulevya pamoja na uuzaji na utumiaji wa pombe za viroba
Nataka kuwaagiza kuwa agizo suala la usimamizi wa Mapato kwa Sasa ni Jambo muhimu sana kwa kila mtu kulichukua na kulifanyia kazi kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha kuwa Mapato ya Serikali hayapotei kwa namna yoyote ile.
Halmashauri ya Wilaya ya Siha inajumla ya Kata 17 na vijiji 60 na Vitongoji 169
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment