baadhi ya madawati yaliyotolewa na Wadau wa maendeleo kutoka Nchini Singapore kwa shule za msingi Wilaya ya Siha. Wadau hao wametoa jumla ya Madawati 100 kwa shule za msingi na kufanya ukarabati wa miundombinu katika shule ya msingi Kilari Kata ya Gararagua Wilayani Siha hivi karibuni
miongoni wa wadau hao kutoka Singapore wakimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Siha choo cha kisasa kwa wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Kilari
Wednesday, 22 June 2016
Tuesday, 21 June 2016
BARAZA MAALUM LA MADIWANI YAKUTANA SIHA
Baraza la Madiwani katika halmshauri ya Wilaya ya Siha yafanya baraza maalum tarehe 17.6.2016 kwa ajili ya kupitia mambo mbalimbali muhimu ya Halmashauri likiwemo la kupitisha wajumbe wawili wa Kamati ya Fedha ,uongozi na Mipango
Baraza hilo la maalum la Madiwani pamoja na mambo mengine agenda muhimu katika kikao hicho ilikuwa ni kupitisha wajumbe wawili waliongezwa katika kamati ya Fedha ,Uongozi na Mipango kwa lengo la kuongeza nguvu katika kamati hiyo
wajumbe waliopendekezwa la baraza hilo ni wafuatao:-
1. Elia Kiwia-Diwani wa Kata ya Ivaeny
2. Claudia Muro-Diwani Viti Maalum Siha
Sunday, 19 June 2016
ASANTE AFRICA YACHANGIA MADAWATI 48 WILAYANI SIHA
Katika kuunga mkono
jitihada za serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania za kupambana na uhaba
wa madawati katika shule za msingi na Sekondari Wilayani siha
Shirika lisilo la
Kiserikali asanteAfrica kutoka nchini Marekani na lenye makao makuu mjini
Arusha Tanzania kwa ukanda huu wa afrika Mashariki limechangia jumla ya madawati 48 Wilayani Siha
yenye thamani ya fedha za Kitanzania shilingi 3.6 milioni.
Akikabidhi msaada huo kwa
Halmashauri ya Siha mwakilishi wa shirika hilo ndugu Tesha alisema kuwa shirika
lake limeamua kuchangia katika madawati ili kunusuru matatizo wanayopata wanafunzi
mashuleni ya kukaa kwa msongamano madarasani.
Alieleza kuwa wakati taifa
linapambana na kuondoa uhaba wa madawati mashuleni,shirika la asante Africa limeona
ni vema kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya rais wa Tanzania Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli.
Alisema kuwa shirika lake
limeona kwa wakati huu ni vema kushirikiana na Serikali katika kuboresha suala
la elimu kwa kutambua kuwa taifa ili lipate maendeleo ya kweli watu wake
wanatakiwa kupata elimu bora na siyo bora elimu,alisema Tesha
Akipokea msaada huo
mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha Rashid Kitambulio alishukuru shirika hilo kwa kuendelea kuunga
mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha suala la elimu kwa
watoto wa kitanzania.
Alieleza kuwa Halmashauri
ya Wilaya ya Siha itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo
kutoka ndani na nje ya nchi ili kuwaletea wananchi wa Siha maendeleo
yanayotakiwa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo suala la elimu
Mkurugenzi wa Siha alieleza
kuwa hadi sasa Halmashauri yake imebakiza kiasi cha madawati 1744 tu ili
kuondoa tatizo hilo katika shule zote za msingi na sekondari Wilayani humo.
Kitambulio aliwataka wadau
wengine wa maendeleo wilayani Siha kuiga mfano wa shirika la AsanteAfrika
katika kuchangia madawati na miundombinu mingine katika shule za msingi na
Sekondari ili kuboresha kiwango cha elimu katika Wilaya ya Siha.
Alielza kuwa Wilaya ya Siha
kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2012 hadi 2015 kiwango cha elimu kimekuwa
kikiendelea kupanda kwa mjongea chanya hasa katika shule za msingi nakuifanya
Halmashauri ya Siha kushika nafasi ya tatu kwa Mkoa wa Kilimanjaro.
Halmashauri ya Wilaya ya
Siha inajumla ya shule za Msingi za Serikali 54 na 13 za Sekondari ambazo
nyingi zinahitaji kuboreshwa zaidi katika miundombinu yake ili kuendana na
wakati na maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia.
ASANTE AFRICA YACHANGIA MADAWATI SIHA
ASANTE
AFRICA YACHANGIA MADAWATI SIHA

Subscribe to:
Posts (Atom)