Wednesday, 7 October 2020
Friday, 2 October 2020
Halmashauri ya Siha yapongezwa na kuboresha stendi ya mabasi Sanya Juuu
Wakazi na Wananchi wa Wilaya ya Siha wameendelea kutoa pongezi kwa Halmashauri ya Siha kwa kuboresha kituo cha Mabasi Sanya Juu. Wanachi hao hasa madereva na wamiliki wa magari ya abiria katika nyakati tofauti wameeleza kufurahishwa na miundombinu bora na imara iliyopo katika stendi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli akiwa na viongozi wa dini hivi karibuni ambapo walitembelea stendi hiyo alieleza kuwa Halmashauri ya Siha imetumia zaidi ya shilingi Milioni 4 ya mapato ya ndani katika kuboresha miundombinu ya Stendi ya Sanya Juu na ile ya KIA.
WANAFUNZI 2357 KUHITIMU ELIMU YA MSINGI SIHA 2020
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli amesema kuwa kati ya wanafunzi 2357 watakaomaliza darasa la saba tarehe 7-8/10/2020 wasichana ni 1230 na wavulana ni 1127 katika shule za msingi 59,Shule za Serikali 53 na za mashirika na dini na binafsi ni shule 06
Maandalizi ya kufanyika kwa mtihani huo yameshakamilika na matarajio ya Halmashauri ni kuendelea kupata matokeo mazuri na kushika nafasi za juu kimkoa na Kitaifa alisema ndugu Ndaki Mhuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha
Subscribe to:
Posts (Atom)